Advertisements

Thursday, June 21, 2018

HABARI KATIKA PICHA

pichani waziri wa Madini Mheshimiwa Angella Jasmine Kairuki akiwapokea na kisha kukaa na wabunge hao kwa lengo la kuwapa ujuzi juu ya usimamizi wa sekta ya madini kwa wachimbaji wadogo wa madini.
Wabunge wa Bunge la Gauteng kutoka Afrika kusini waja Tanzania kujifunza juu ya usimamizi wa wachimbaji wadogo wa madini .
Majira ya mchana Ujumbe wa watu tisa walifika katika ofisi ya Waziri wa Madini jijini Dodoma na kujifunza mambo mbalimbali kama vile mabadiliko ya sheria ya madini , usimamiaji wa sheria ya wachimbaji wadogo, sera ya madini kwa wachimbaji wadogo , pamoja na namna ya kuzuia uchimbaji haramu , namna ya kuzuia utoroshwaji wa madini , namna ya kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wachimbaji wadogo, jinsi ya kuwawezesha wachimbaji wadogo, jinsi ya kutafuta masoko na fedha za kuwawezesha katika uchimbaji, uanzishwaji wa vyama vya wachimbaji wadogo pamoja na ushiriki wao katika maamuzi ya kitaifa.
mkutano huo uliwashirikisha pia manaibu waziri wa madini pamoja na mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Iddris Kikula
Picha ya pamoja

No comments: