Advertisements

Monday, June 18, 2018

Kisa bia kipa Misri akataa tuzo mchezaji bora wa mechi

Moscow, Russia. Kipa wa Misri, Mohamed El-Shenawy alikataa kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya Kombe la Dunia katika Kundi dhidi ya Uruguay kwa sababu inadhaminiwa na kampuni Budweiser.

El-Shenawy alionyesha kiwango cha juu kuokoa mashuti ya washambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavan na Luis Suarez kabla ya Jose Gimenez kufunga bao dakika ya 89.

Pamoja na kufungwa, kiwango cha El-Shenawy kiliwalazimisha wasimamizi wa tuzo ya MOTM kumteua kipa huyo wa Misri kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo ya Kundi A iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ekaterinburg.

Lakini wakati anakabidhi kipa huyo wa El Ahly alikataa kuipokea kwa sababu wadhamini hao ni kampuni kubwa ya kutegeneza bia ya Budweiser.

El-Shenawy ni Muislamu kutoka na imani yake kupiga marufuku kabisa matumizi ya pombe hivyo aliamu kukataa kupokea tuzo hiyo.


Budweiser ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Kombe la Dunia 2018, Russia wamesaini mkataba na FIFA kusambaza bia katika mashindano hayo.

MWANASPOTI

No comments: