WASHINDI WA TUZO ZA MO
SIMBA 2018
1.
GOLIKIPA BORA WA MWAKA
A.
Aishi Manula - WINNER
B. Said Mohamed 'Nduda'
C. Emmanuel
Elias Mseja
2.
BEKI BORA WA MWAKA
A. Yusuph Mlipili
B.
Erasto Nyoni - WINNER
C. Shomari Kapombe
3. KIUNGO BORA WA MWAKA
A. Jonas Mkude
B. James Kotei
C.
Shiza Kichuya – WINNER
4.
MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA
A.
Emmanuel Okwi - WINNER
B. John Bocco
C. Shiza Kichuya
5. MCHEZAJI BORA MWANAMKE WA MWAKA
A. Rukhia Salum
B.
Zainabu Rashidi Pazzi - WINNER
C. Dotto Makunja
6.
MCHEZAJI BORA MDOGO WA MWAKA
A. Ally Salim (GK)
B.
Rashid Juma – WINNER
C. Salumu Shabani
7. GOLI BORA LA MWAKA
-
John
Bocco (Simba VS Mwadui)
8.
TUZO YA BENCHI LA UFUNDI
A. Pierre Lechantre – Kocha Mkuu
B. Masoud Djuma – Kocha Msaidizi
C. Mohamed Aymen – Kocha wa Viungo
D. Muharam Mohamed – Kipa wa Makipa
E. Richard Robert – Meneja wa Timu
F. Yassin Gembe – Daktari wa Timu
G. Abbas Selemani – Mratibu
9. SHABIKI BORA WA MWAKA
- Fihi Salehe Kambi
10. MHAMASISHAJI BORA WA MWAKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
A.
Hamis Mwinjuma (Mwana FA) - WINNER
B. Salama Jabir – WINNER
C. Zitto Kabwe
D. Vyonne Cherrie (Monalisa)
E. Omary Nyembo (Ommy Dimpoz)
11. MHAMASISHAJI BORA
- Haji Manara
12. TAWI BORA LA MWAKA
A. Wazo Hill
B.
Ubungo Terminal - WINNER
C. Vuvuzela
13. KIONGOZI BORA WA MWAKA
- Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah Muhene
14. TUZO YA WASIMAMIZI WA MCHAKATO WA MABADILIKO
A. Jaji Mstaafu Thomasi Mihayo
B. Wakili Damasi Ndumbaro
C. Abdulrazak Badru
D. Mussa Hassan Zungu
E. Yusuph Nassoro
F. Brenda Mrema
G. Mzee Hamis Boma
H. Revocatus Cosmas Sangu
I. Hashim Nyendage
J. Gervas Alpha Honest
K. Emmanuel Metusela Urembo
L. Mulamu Nghambi
M. Selemani Omari
N. Aziz Kifile
O. Salim Abdallah Muhene
P. Arnold Kashembe
Q. Omari Bakari Mtika
R. Evodius Mtawala
15. TUZO YA HESHIMA
(LIFETIME ACHIEVEMENT)
- Selemani
Matola – WINNER
16. MCHEZAJI BORA WA MWAKA
A.
Emmanuel
Okwi
B. John Bocco - WINNER
C.
Shiza
Kichuya
MHE MGENI RASMI, DKT.
HAMISI KIGWANGALLA, WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,
MHE MGENI MAALUMU, MZEE
WETU ALI HASSAN MWINYI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KAIMU RAIS WA SIMBA,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA
SERIKALI,
WAHESHIMIWA WABUNGE,
WAHESHIMIWA MABALOZI,
WAJUMBE WA KAMATI WA
UTENDAJI YA KLABU YA SIMBA,
VIONGOZI WA TFF,
VIONGOZI WA BODI YA LIGI,
VIONGOZI WA BARAZA LA
MICHEZO LA TAIFA,
WADHAMAINI WA KLABU YA
SIMBA,
MWENYEKITI NA WAJUMBE WA
KAMATI YA ZABUNI YA KLABU YA SIMBA,
WAJUMBE WA KAMATI YA UWEKEZAJI
YA KLABU YA SIMBA,
WANACHAMA WENZANGU,
MARAFIKI ZANGU,
WANAHABARI,
WAGENI WAALIKWA MABIBI NA
MABWANA
ASALAAM ALAYKUM.
SIMBA… (NGUVU MOJA)
SIMBA… (NGUVU MOJA)
THIS IS… (SIMBA)
AWALI YA YOTE TUMSHUKURU
SANA MWENYEZI MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUFIKIA SIKU HII YA LEO. NI SIKU KUBWA SANA
KWETU KWENYE SHEREHE HII YA TUZO KWA WATU WALIOI-WEZESHA KLABU YETU YA SIMBA
KUFIKA HAPA ILIPO SASA.
KIPEKEE, TUMSHUKURU TENA
MWENYEZI MUNGU AMBAYE AMETUWEZESHA KWA MATAKWA YAKE KWA MARA YA KWANZA KUKUTANA
BAADA YA KUSHINDA ZABUNI KATIKA KLABU YETU YA SIMBA. NA KUANDAA TUZO AMBAZO
ZITAKA-ZOTOLEWA KWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI NA WAPENZI
MBALIMBALI WA SIMBA.
NICHUKUE NAFASI HII
KUISHUKURU SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INAYOONGWA NA MHE. RAIS
DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA JITIHADA ZA KUSAIDIA NA KUKUZA UCHUMI WETU, AMBAO
KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, UMETOA FURSA KWETU SISI KUWEZA KUWEKEZA KATIKA MAENEO
MBALIMBALI IKIWEPO KATIKA KLABU HII. LAKINI PIA KUWASHUKURU WASAIDIZI WAKE
KUANZIA MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI WOTE KWA KAZI KUBWA WANAYOI-FANYA
YA KULIJENGA TAIFA HILI.
MHE. MGENI RASMI NA
WAGENI WAALIKWA, KAMA MNAVYOFAHAMU KWAMBA KLABU YETU YA SIMBA IMEINGIA KATIKA
MFUMO MPYA WA UENDESHAJI AMBAO UMETUPA NAFASI YA KUWEKEZA KATIKA KLABU HII TUNAYOISHABIKIA
SANA.
MARA KADHAA NA HASA
KATIKA KIPINDI HIKI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, NIMEKUWA NIKITUMIA SEHEMU
YA MUDA WANGU KUJIULIZA? KWANINI MUNGU AMENIFANYA NIWE NA MAPENZI MAKUBWA KIASI
HIKI NA KLABU HII.? LAKINI NAAMINI HILI NI JUKUMU AMBALO NIMEPEWA NA MWENYEZI
MUNGU ILI NIIFANYIE MAZURI KLABU HII.
KLABU YETU INA HISTORIA
KUBWA KATIKA SOKA LA HAPA NCHINI, AFRIKA MASHARIKI, NA AFRIKA KWA UJUMLA,
LAKINI HATUKUWA NA UTARATIBU WA KUTOA TUZO KWA WENZETU AMBAO WALIJITOA KWA MOYO
WAO WOTE, ILI KUHAKIKISHA TUNAPATA MAFANIKIO KATIKA MICHUANO MBALIMBALI AMBAYO
TUNASHIRIKI.
KUNA MASHABIKI WAMEPOTEZA
MAISHA YAO KWA AJILI YA SIMBA. KUNA MASHABIKI WANATUMIA SEHEMU KUBWA YA MUDA
WAO KWA AJILI YA SIMBA. KUNA VIONGOZI WANAFANYA KAZI KWA BIDII SANA ILI TU.
SIMBA IFANIKIWE. KUNA WACHEZAJI WETU WANACHEZA KWA KUJITUMA SANA, ILI SIMBA
IPATE MAFANIKIO. KUNA BENCHI LA UFUNDI AMBALO LINAHAKIKISHA LINATUMIA KILA
MBINU ILI TU TUPATE MATOKEO MAZURI.
KWA MFANO, TULIKUWA NAYE
MCHEZAJI WETU MAREHEMU HUSSEIN TINDWA, AMBAYE ALIFARIKI DUNIA NDANI YA UWANJA,
HUKU AKIITUMIKIA KLABU YETU ILIPO KUWA IKICHEZA NA MABINGWA WA ZAMANI WA
NIGERIA, KLABU YA RACCAH ROVERS MWAKA 1979. HUYU TUNA KILA SABABU YA KUMKUMBUKA,
YEYE NA WENGINE KAMA OTHMAN MAMBOSASA, OMARI MAHADHI BIN JABIL, PATRICK
MAFISANGO, MOHAMED KAJOLE, ADAMU SABU, EDWARD CHUMILA, MARTIN KIKWA, NA
WACHEZAJI WENGINE WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI. MUNGU AWAREHEMU NA AZILAZE
ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI. AMEEN
KWA RUKHSA YAKO MHE.
MGENI RASMI NAOMBA TUSIMAME KWA DAKIKA MOJA ILI TUWAENZI NA KUWAKUMBUKA PAMOJA
NA KUTOA HESHIMA KWA MALEGENDARIES WETU HAWA.
PAMOJA NA NYOTA WETU HAWA
WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI, KLABU YA SIMBA IMETOA NYOTA WENGI SANA KUANZIA
KARNE ILIYOPITA MIAKA YA 60 MPAKA HIVI LEO. MIONGONI MWAO NI MBARAKA MOHAMED,
ABDALLAH KIBADEN, MTEMI RAMADHANI, ZAMOYONI MOGELA, MALOTA SOMA (BALL JUGGLER),
SELEMANI MATOLA NA WENGINE AMBAO HAKUNA ASIYEJUA WALICHOI-FANYIA SIMBA NA TAIFA
HILI KWA UJUMLA.
ILINICHUKUA MUDA KUFIKIRIA
NI JAMBO GANI TUNAWEZA KUWAFANYIA WENZETU WALIO-ITENDEA MAMBO MAKUBWA KLABU. NA
PIA KUWAINSPIRE WACHEZAJI WETU WA SASA, ILI WAWEZE KUJUA THAMANI YA KUCHEZEA
SIMBA NA UKUBWA WA KLABU HII. HAPO NDIPO WAZO LA KUTOA TUZO ZA MO SIMBA
LILINIJIA. NINAAMINI KWAMBA HII ITAKUWA NI NJIA BORA SANA YA KUTAMBUA MCHANGO
WAO AMBAO UMEIWEZESHA SIMBA KUFIKA HAPA BAADA YA MIAKA 81 TANGU KUANZISHWA
KWAKE.
HAIKUWA KAZI RAHISI,
KWANI BAADA YA KUPATA WAZO LA TUZO NILIKUWA NA KAZI NYINGINE YA KUHAKIKISHA
KUNAKUWA NA VIPENGELE AMBAVYO VITAGUSA KILA SEHEMU KWA WATU AMBAO JUHUDI ZAO ZIMESAIDIA
SIMBA KUFIKA HAPA, KUANZIA KWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI
NA MATAWI YA SIMBA.
ILIKUWA KAZI KWELIKWELI,
NA BAADAE NILIPATA VIPENGELE 16 AMBAVYO KWA HAKIKA VITAMGUSA KILA MMOJA WETU
KUTOKANA NA JUHUDI ZAKE KWENYE KLABU HII.
ILI KUPATA WASHINDI
HALALI, TULIONA NI VYEMA KAZI YA KUCHAGUA WASHINDI NIWAACHIE MASHABIKI WENZANGU
AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUPIGA KURA KUPITIA TOVUTI YA MOSIMBAAWARDS.CO.TZ NA KURASA
ZA SIMBA ZA TWITTER, FACEBOOK NA INSTAGRAM. LAKINI PIA TULITEUA KAMATI AMBAYO
ILIHUSISHA WADAU MBALIMBALI WA SOKA HAPA NCHINI KAMA TFF, BODI YA LIGI, MAKOCHA
WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA, WACHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA, WADHAMINI NA
WANAHABARI. NA KATIKA HILI NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUISHUKURU KAMATI KWA
KAZI KUBWA WALIYOIFANYA USIKU NA MCHANA ILI KUHAKIKISHA SHUGHULI HII
INAFANIKIWA.
USHINDANI ULIKUWA NI
MKUBWA SANA, HIVYO KILA KIPENGELE WALICHAGULIWA WATU WATATU, NA HII HAIMAANISHI
KWAMBA AMBAO HAWAKUPATA NAFASI YA KUJUMUISHWA KATIKA VIPENGELE VYA TUZO ZA MWAKA
HUU KUWA SIO BORA, BALI ILIKUWA NI LAZIMA KILA KIPENGELE WAPATIKANE WATU WATATU
KWA AJILI YA KUPIGIWA KURA.
KWANI KAMA MNAVYOFAHAMU
TIMU YETU INA WACHEZAJI WENGI WENYE VIWANGO AMBAVYO HAVIPISHANI SANA. HIVYO
USHINDANI ULIKUWA NI MKUBWA, LAKINI MWISHO WA SIKU LAZIMA MSHINDI APATIKANE.
BAADHI YA VIPENGELE AMBAVYO VILIKUWA NA USHINDANI MKUBWA NI KIPENGELE CHA
MCHEZAJI BORA NA GOLI BORA, KWANI TULITOA NAFASI KWA MASHABIKI WENYEWE NDIO
WACHAGUE.
NAOMBA NITUMIE NAFASI HII
KUWAOMBA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI NA MASHABIKI, AMBAO WATASHINDA
TUZO TUNATEGEMEA KUONA MKIZIDI KUONGEZA JUHUDI ZAIDI ILI KLABU YETU IZIDI
KUSONGA MBELE KWA KUPATA MAFANIKIO. NA KWA AMBAO WATAKOSA NIWATIE MOYO KWAMBA
HUU SIO MWISHO WA TUZO HIZI. ZITAKUWEPO KILA MWAKA INSHALLAH, HIVYO MKIJITUMA
ZAIDI LABDA MWAKANI MNAWEZA KUWA MOJA YA WASHINDI WA TUZO KATIKA VIPENGELE
MBALIMBALI AMBAVYO TUTAVIWEKA.
MWISHO, NAPENDA
KUWASHUKURU WATU WOTE TULIOWAALIKA KWA KUKUBALI KUITIKIA MWITO WETU. MWENYEZI
MUNGU AWAJALIE. MUNGU IBARIKI SIMBA. MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI
AFRIKA.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA…
THIS IS… (SIMBA)
No comments:
Post a Comment