Advertisements

Tuesday, June 12, 2018

Mbowe, Lowassa watinga mahakamani

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema, wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe inaendelea muda huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Waziri Mkuu wa Mstaafu, Edward Lowassa ametinga katika mahakama hiyo, akiambatana na viongozi wa chama, akiwemo Mbowe.

Wengine walioingia mahakamani hapo ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu John Mnyika (Bara), Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu (Zanzibar) na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Soma Zaidi: Kibatala awasilisha kusudio la kukata rufaa kesi ya Mbowe, vigogo Chadema

Wanakabiliwa na mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo ya kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali na kuhamasisha maandamano yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

No comments: