Advertisements

Sunday, June 10, 2018

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KURUDIWA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA USHIRIKA KILA MAHALI PENYE DOSARI WILAYANI IKUNGI

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi wakati wa ziara ya kukagua vituo vya ununuzi na ukusanyaji wa pamba Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WK
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akishuhudia ununuzi na ukusanyaji wa pamba baada ya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza akiwasikiliza kwa makini maswali ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio kabla ya kumkaribisha Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba , Jana 8 juni 2018.
Waziri wa kilimo akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Singida.
Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa hadhara

Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Afisa ushirika wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Ndg Gurisha Msemo kufanya ziara ya kikazi maeneo yote kuliko fanyika uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika ili kubaini uhalali wa uwepo wao.

Mhe Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya wakazi wa Kijiji cha Mkunguakihendo na Misughaa Wilayani Ikungi kuonyesha kutotambua namna walivyochaguliwa viongozi waliopo madarakani kukiongoza chama hicho katika ngazi mbalimbali jambo ambalo lina ashiria kupatikana kwa viongozi hao kinyume na utaratibu.

Dkt Tizeba ameyasema hayo jana 8 Juni 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida.

“Pamoja na maelekezo yangu ya kutazamwa mahali penye matatizo na kufanyika upya uchaguzi lakini pia nawasihi pindi utakapofanyika uchaguzi mchague viongozi waadilifu ambao watawasimamia katika kweli na haki”

“Kwa muda mrefu sana kwenye vyama vya ushirika karibu nchi nzima watu walikuwa wanagawana vyeo badala ya kuchagua viongozi bora kwa maslahi ya wananchi, lakini katika kipindi hiki tumedhamiria kwa dhati kabisa kuwa na haki katika upatikanaji wa viongozi wa chama chenu” Alikaririwa Mhe Tizeba

Sambamba na agizo hilo pia amewasihi viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika kote nchini kutojihusisha na wizi wa fedha za wananchi kwani kufanya hivyo sio kosa la wizi pekee bali ni kosa la uhujumu uchumi.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu  amewasihi maafisa ugani kuongeza ufanisi katika usimamizi kwenye kilimo ili kuongeza tija itakayopelekea kuwa na mavuno mazuri yenye manufaa makubwa kwa wakulima.

Aliwaomba wataalamu wa utafiti kote nchini kupitia upya katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini dawa bora za kuua wadudu wanaoathiri mazao mbalimbali likiwemo zao la pamba.

No comments: