Advertisements

Monday, July 9, 2018

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumchoma Moto wa Pasi Kijana Aliyekuwa Anamvizia Binti Yake

Mkazi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Nikodemu Johnson amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga na kumchoma kwa pasi ya umeme kijana mmoja mkazi wa Katesh aliyemkuta ndani ya nyumba na binti yake.

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu wa Wilaya Amani Petro Shao.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa Mei 28 mshtakiwa alimpiga na kumchoma kwa pasi ya umeme Christopher Bayanga (19) baada ya kumkuta kijana huyo kwenye nyumba ya mtuhumiwa.

Alidai kipigo alichomfanyia kijana huyo, hasa kuchomwa kwa pasi ya moto, kimemsababishia maumivu makali na kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kwani alifungiwa ndani wakati huo. Johnson yuko nje kwa dhamana hadi Julai 25 wakati kesi hiyo itakaposikilizwa.

No comments: