Advertisements

Monday, July 9, 2018

Gigy Money Azimikia Umbo la Vanessa Mdee

Msanii wa Bongo fleva Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutiwa sana na umbo la msanii mwenzake Vanessa Mdee.

Moja kati ya vitu ambavyo vilitengeneza headlines kuhusu Gigy Money ni kupungua ghafla kwa mwili wake na kuzua tetesi kuwa anaumwa na maneno mengine mengine.
 
Lakini Kwenye mahojiano na Clouds Fm, Gigy Money amesema hivi sasa anajithidi kupunguza mwili wake ili aweze kutumbuiza vizuri jukwaani kama anavyofanya Vanessa Mdee.

"Kuna muonekano wa show tofauti na picha za Instagram mimi sasa hivi ni performer, huwezi kwenda jukwaani una limwili lako tu. Kwa hiyo mtu unatakiwa na mwili fulani hivi”.

"Do you look Vanessa akiwa ana-perform, how do you feel unaoana kabisa machachari, anaweza kuwa na bendi, anaweza kuinua mguu, unafurahi, sio mtu shabiki anasubiri utikise makalio tu”.

Siku chache zilizopita Gigy Money alikiri kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka apungue mwili ni mapenzi ambapo alikuwa anaumizwa na penzi la Baba watoto wake Mo J.

No comments: