Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifuatilia kwa kutumia darubini mazoezi kwa vitendo katika Ziwa Viktoria Mwanza yaliyokuwa yakioneshwa na askari waliohitimu mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza.Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Mary Tesha. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wanafunzi waliohitimu mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza baada ya kuangalia Onesho lao la utayari katika ukanda wa Ziwa Viktoria Mwanza.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Mary Tesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Polisi Wanamaji yaliyokuwa yakiendeshwa katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifanya mazoezi mafupi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mwanza baada ya Askari hao kuonyesha zoezi lao la utayari wakati wa Ziara ya IGP mkoani humo.
Askari Polisi wakionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kupitia kwa vitendo katika Ziwa Viktoria Mwanza wakati wa kufunga mafunzo yao katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza. (Picha na Jeshi la Polisi)
No comments:
Post a Comment