ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 3, 2018

Magufuli amtaka Mengi kutafsiri kitabu chake kwa Kiswahili

 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinchaoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, Dk. Jane Goodall (katikati) pamoja na Mbunge wa zamani wa Kahama, Mh. James Lembeli (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akifurahia kuwaona baadhi ya marafiki wa karibu kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Kutoka kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,  Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kinachoitwa  “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mke wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Prof Rwakaza Mukandara wakati wakisubiri kuwasili kwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu cha mumewe kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” katika hafla iliyotia fora kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimtambulisha mmoja kati ya washindi wawili wa wazo la kibiashara la shindano la kujenga hoja asili ya ujasiriamali lililojulikana kama “DREAM TO GREATNESS“ Wakonda Kapunda (anayesukumwa kwenye baiskeli) kabla ya kumkabidhi zawadi ya dola za kimarekani 20,000 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi  akizungumziakuhusu  msukumo wa kuandika kitabu hicho cha historia ya maisha yake ili kutimiza azma ya marehemu mtoto wake Rodney Mutie Mengi (kwenye back ground pichani) aliyemtaka kuandika kitabu hicho na mambo mengine ambayo atayatimiza kadri awezavyo kumuenzi mtoto wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu chake hicho kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani)  kinachoitwa“I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na mgeni rasmi Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Prof Rwakaza Mukandara akitoa muhtasari wa kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani)  kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Pichani ni ukumbi wa Marquee wa hoteli ya Serena jijini Dar es Saalaam ukiwa umefurika watu mashuhuri na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani)  “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kilichozinduliwa na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
 Watoto Mapacha Jayden na Ryan wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi wakimkabidhi Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Magufuli kitabu kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kwa ajili ya kukizindua rasmi katika hafla iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimueleza jambo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Magufuli kuhusu kitabu chake kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” kabla ya kukata utepe kukizindua. Waliopamba uzindizi huo ni Watoto mapacha Jayden na Ryan Mengi wakati wa hafla iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Magufuli akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,  Dk. Reginald Mengi kabla ya kukata utepe kuzindua kitabu cha Mwenyekiti huyo kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” wakati wa hafla iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mke wa Dk. Mengi, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na watoto wao mapacha Jayden na Ryan Mengi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizundua kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” katika halfa iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, Dk. Jane Goodall (kulia), Mke wa Dk. Mengi, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kulia) pamoja na watoto mapacha wa Dk. Mengi Jayden na Ryan Mengi.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi ambaye pia ni mtunzi wa kitabu cha “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” akifunua ukurasa maalum aliomuandikia ujumbe Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kukizundua rasmi kitabu hicho kinachopatikana katika ‘book stores’ na mtandao wa Amazon. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, Dkt. Jane Goodall (kulia), Mke wa Dk. Mengi, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kulia) pamoja na watoto mapacha wa Dkt. Mengi Jayden na Ryan Mengi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi nakala ya kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi kinachoitwa “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” mara baada ya kukizindua katika hafla iliyofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na meza kuu katika picha ya pamoja na wanafamilia ya Mengi kwenye uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi  baada ya kukizindua katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.
Pichani juu na chini ni viongozi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi, chama, dini na taasisi mbalimbali nao waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.

Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mh. Dk.  John Pombe Magufuli amemuomba mfanyabiashara maarufu nchini Dk. Reginald Mengi kutafsiri kitabu chake alichokizundua jana ili kiweze kuwasaidia wananchi wa Tanzania kutambua juhudi zake na kuiga nyayo.
Pamoja na kuhimiza kitabu hicho kuandikwa kwa Kiswahili aliwataka wananchi kununua kitabu  kinachopatikana kwenye maduka yote ya vitabu nchini na on-line kupitia Amazon na kuwasihi Watanzania wengine kukisoma. Kitabu hicho kimeaandikwa kwa Kiingereza.
Aidha aliwataka Watanzania kuepuka tabia za kukatishana tamaa katika kupanga, kuamua na kutekeleza shughuli za kujiletea maendeleo binafsi na ya taifa.
Alisema Mzee Mengi alikatishwa tamaa katika mambo mengi ambayo yalipita katika maisha yake ikiwamo katika masuala ya madini. Aliwataka watanzania kujiamini kama mzee Mengi alivyojiamini na kufika hapo.
Akizindua kitabu cha Dkt. Reginald Mengi kiitwacho 'I Can, I Must, I Will' ambacho kwa Kiswahili kingeitwa 'Ninaweza, Ninalazimika, Nitafanikiwa.'katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam, kukatishana tama kunazuia maendeleo ya watu binafsi na taifa.
Kitabu hicho ambacho kinaelezea maisha ya Dk. Mengi, chenye sura 10 kina jumla ya kurasa 311.
Dkt. Magufuli alisema tabia hiyo ya kukatishana tamaa ipo pia ndani ya Serikali na huko ni kukubwa sana.
Katika hilo akitolea mfano kuwa hata wakati Serikali yake ilipoamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu bure, kuna watu walisema jambo hilohaliwezekani kwa kuwa hata Ulaya na Marekani watu hawasomi bure.
Dk. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake ilishikiliamsimamo huo wa kutoa elimu bure ambao umezaa matunda kwa kuwa ilipofikia Novemba mwaka 2015, ilianza kwa kutoa Sh bilioni 23.58 kila mwezi ambazo zilipelekwa shuleni moja kwa moja.
Alisema kitendo hicho cha kutoa elimu bure kiliwezesha kuongeza idadi ya watoto walioandikishwa darasa la kwanza kuongezeka kutoka milioni moja hadi kufikia watoto milioni 1.98.
"Hata tulipotaka kujenge reli ya kisasa (SGR) ili bandari itumike vizuri… na kuifufua Kampuni yetu ya ndege kwa kununua ndege mpya, pamoja na kutaka kuzalisha umeme kule Stiegler's Gorge, kuna watu walipinga na kusema mambo hayo hayawezekani, lakini sasa tumeweza kuanza kujenga reli ya kisasa lakini pia tumenunua ndege mpya saba tena kwa fedha zetu,"alieleza Dk. Magufuli.
Tuliambiwa hatuwezi kwa kuwa iliwashinda wengine kwa kuwa ilijengwa miaka 100 iliyopita na Wajerumani na waingereza wakamalizia kwa hiyo ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kama wale walijenga kidogo kidogo kwanini na sisi tusijenge? ndio tumeanza kujenga kilomita 769 kwa gharama za ndani.
Tumeanza kazi na ndio sasa wanakuja kusema watatukopesha kwa sababu wanaona kwamba tunaweza, we can.
Alisema pamoja na kuvunjwa moyo huo serikali yake imechukua hatua za kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya kimkakati kuwezesha matumizi ya bandari ya Dar es salaam na kasi ya usafirishaji wa mizigo.
Pamoja na kusema kwamba wakatishaji tama wapo wengi aliwataka Watanzania kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Dk. Mengi katika kujikwamua na umaskini kwa kusoma kwa bidii ili kupata maarifa mapya na kufanya kazi kwa bidii kama alivyofanya Dk. Mengi kufikia kuwa mfanyabiashara mkubwa Afrika Mashariki na Kati.
Rais Magufuli aliwataka Watanzania kujifunza mambo mengi kutoka kwenye kitabu hicho cha Dk. Mengi, ikiwamo kufanya kazi kwa bidii pamoja na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo yakiwemo maneno ya kukatisha tamaa.
Kwa upande wake Dk. Mengi alisema pamoja na kutoka katika familia maskini, hakukata tamaa na badala yake alijifunza kutoka kwa wazazi wake na kaka yake waliojituma kwa hali na mali ili familia yao iondokane na umaskini.
Dk.  Mengi alisema kuwa baba yake alikuwa akifanya kazi ya kununua kondoo waliokonda na kisha kuwasafisha kwa maji na kuwauza tena kwa bei ya juu, na hivyo hivyo ilikuwa kwa mama yake ambaye naye alikuwa akinunua ulezi na kuutia maji kisha kuuza tena kwa faida.
Aliongeza kuwa mafanikio yake pia yalichangiwa na tabia ya kaka yake ya kujituma katika kufanya biashara ya mayai kwa kuanza kuuza mayai manne, lakini pia alifanya kazi ya kusafisha viatu vya askari na kulipwa hadi alipopata mtaji wa kufungua biashara kubwa na akafanikiwa.
"Nilitoka katika familia maskini, tulikuwa tunalala kwenye nyumba ya udongo tena chini, lakini sikukata tamaa, kuzindua kitabu hiki leo, ni kutimiza ndoto ya marehemu mwanangu Rodney, aliyenitaka kuandika kitabu kitakachoelezea maisha yangu tangu mwanzo hadi kufanikiwa kwangu," alieleza Dk. Mengi.
Katika uzinduzi huo wa kitabu, Dk. Mengi pia alitoa zawadi ya dola za Marekani kwa washindi wawili walioweza kuandika mawazo mazuri ya kibiashara.
Washindi hao ambao ni Wakonta Kapunda kutoka Tanzania na Bryan Mwenda kutoka Kenya, kila mmoja alipewa hundi ya dola za Marekani elfu 20.
Rais Magufuli pia aliamzawadia Wakonta, Sh milioni 10 ili zimsaidie katika kufikia ndoto zake za kimaisha.
Mbali na Dk. Magufuli ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, dini na taasisi mbalimbali nao walihudhuria kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya viongozi hao ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Naibu Spika Dk. Tulia Ackson, mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalam.

No comments: