Advertisements

Friday, July 6, 2018

Mwili wa Patrick wawasili, wahifadhiwa hospitali Aga Khan

Mwili wa mtoto wa muigizaji wa filamu nchini, Muna love, Patrick Peter, umewasili nchini leo saa 11:45 na kupelekwa hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Akizungumza na MCL Digital, leo Julai 6. msemaji wa familia, Banzo Peter amesema,mwili umewasili saa 11:45 jioni na ndege ya Shirika la Kenya Airways(KQ).
Mwili huo uliondoka Kenya saa 9:40 jioni.
Bonzo amesema,baada mwili huo kuwasili ratiba zitaendelea kama zilivyopangwa hapo awali.
"Tunashukuru mwili umeshawasili, na tayari tumeshaupeleka Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa. Niwaambie tu watu ratiba iko vilevile, kesho mwili utakuja nyumbani kwa baba wa mtoto Mwananyamala kwa ajili ya kuagwa na baadae utaagwa viwanja vya Leaders na utazikwa makaburi ya kinondoni, "amesema Bazo.
Patrick alifariki Julai 3, 2018 Nairobi, Kenya alipokuwa akipata matibabu. Familia imesema alikuwa na uvimbe kichwani.

No comments: