Advertisements

Sunday, July 1, 2018

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO BALAZA LA MAWAZIRI, MWIGULU NJE

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akitangaza majina ya Viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Rais John Magufuli leo amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama ifuatavyo:

Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.

Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo mchana huu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.

Taarifa hiyo imesema kwamba nafasi  ya Kangi Lugola inaenda kuchukuliwa na Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mussa Ramadhan Sima.

Aidha Rais amefanya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhumu wa Wizara hiyo ambapo, Mbunge wa Morogoro Kusini Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.

Pamoja na hayo, katika mabadiliko hayo madogo, Rais Mgufuli amefanya Uhamisho Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Hata hivyo Balozi Kijazi amesema tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye

No comments: