ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 21, 2018

UNESCO waendesha kongamano la utawala kwa redio za jamii


 Mwezeshaji kutoka Sung Consultants Wakili, Harold Sungusia akiwasilisha mada juu ya masuala ya uongozi kwenye mafunzo ya siku tano ya uongozi, utawala na menejimenti jijini Dodoma.  Mafunzo hayo yanaratibiwa na UNESCO kwa ufadhili wa SDC.  Mafunzo hayo yanajumuisha wamiliki na mameneja wa redio za kijamii ambazo ni  wanachama wa Mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii (TADIO).
 Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Jukwaa la Wahariri ambao waliwatembelea na kuongea nao.


SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeendesha kongamano la siku tano lenye lengo la kufunza menejimenti, uongozi na utawala  kwa mtandao wa redio za jamii nchini (TADIO).
Kongamano hilo limefanyika Jijini Dodoma kuanzia Julai 17 – 21 .
Kwa mujibu wa UNESCO mafunzo hayo yamelenga kuimarisha mtandao huo.
Mafunzo hayo yalifanywa kwa ajili ya watumishi muhimu wa radio hizo, bodi ya mtandao, sekretarieti ya mtandao na wawakiklishi wa radio wanachama.
Lengo ni kusaidia redio hizo kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu.
Mafunzo hayo yametokana na utafiti uliofanywa kuhusu menejimenti na uongozi wa TADIO katika utekelezaji wake wa majumumu hasa kufuatia malengo ya uwapo wa radio hizo.
UNESCO ikisaidiwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) kwa ufadhili wa Empowering Local Radio kupitia tehama imetoa mafunzo hayo yenye lengo la kuinua ubora wa kazi za redio hizo.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi unaowezesha redio 25 za kijamii zilizo wanachama wa TADIO kuhakikisha kwamba wanatoa huduma zitakazowezesha watu maskini, wanawake na wasichana kuwezeshwa kufanya maamuzi sahihi kwa mambo yanayowagusa kwa kuzingatia taarifa wanazopata kupitia redio hizo.
Pamoja na mafunzo hayo UNESCO pia inajipanga kusaidia menejimenti ya  TADIO na miundombinu yake ili kuweza kutoa huduma bora, kutengenezwa majukwaa elimu na mashirikiano.
TADIO inawanachama wa vituo vya habari na mikutano; vilabu vya waandishi wa habari na radio jamii.
Mtandao huo unaendeshwa na Mkutano Mkuu ambao ndio wenye maamuzi katika masuala yote ya uwajibikaji na utendaji wa sehemu mbaliombali za TADIO; Bodi na sekretarieti inayoendesha shughuli za kila siku za mtandao.

No comments: