Waziri wa Madini ,Angela Kairuki akisalimiana na wakazi wa kata ya Ruvu Kajiungeni alipowatembelea kutoa pole na msaada kufuatia Nyumba zao kuathirika na Mafuriko .
Waziri wa Madini ,Angela Kairuki akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Senyamule wakati akiwafariji wahanga wa mafuriko wilayani Same.
Waziri wa Madini ,Angela Kairuki akizungumza na wakazi katika eneo la Kombo alipofika kutoa pole na Msaada wa Blanketi na Mahemakwa ajili ya kujisitiri.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri Kairuki.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ,Jaseen Al Najem akizungumza wakati wa kukabidhi Msaada wa Chakula kwa wahanga wa Mafuriko katika Kata ya Ruvu Kajiungeni .
Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akitoa taarifa kwa Waziri Kairuki namna ambavyo serikali ya wilaya na mkoa zilivyoshiriki katika kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko katika wilaya ya Same.
Waziri wa Madini,Angela Kairuki akiteta jambo na Balozi wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada kwa wahanga wa Mafuriko.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Madini ,Angela Kairuki aliyeongozana na Balozi wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem kutoa msaada kwa Wahanga hao.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ,Jaseen Al Najem akikabidhi msaada wa Chakula kwa wananchi wa eneo la Kombo wilayani Same.kushoto ni Waziri wa Madini,Angela Kairuki na Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule.
Waziri wa Madini,Angela Kairuki akikabidhi msaada wa Blanketi na Maturubai kwa ajili ya kujengengea mahema ya muda kwa wahanga wa Mafuriko katika wilaya ya Same.
Baadhi ya wakazi wa eneo la Kombo wakiwa wamebeba Vifurushi vya Chakula baada ya kupata mgao kutoka kwa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania zikiwa ni jitihada za Waziri wa Madini ,Angela Kairuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Waziri wa Madini,Angela Kairuki akisalimiana na mmoja wa Wazee ambao kwa sasa wanahifadhiwa na Majirani baada ya nyumba yake kuzingirwa na Mafuriko .
Na Dixon Busagaga,Same.
UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umetoa jumla ya
tani saba za msaada wa Chakula kwa waathirika wa Mafuriko wilayani Same mkoani
Kilimanjaro ambao walilazimika kuyahama makazi yao katia Vijiji vya Kajiungeni
na Ruvu Marwa na kuhamishiwa katika Makambi.
Msaada
huyo uliowasilishwa na Balozi na Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem unatokana na
jitihada za Waziri wa Madini ,Angela Kairuki za kusaidia kaya zilizofikwa na
athari ya mafuriko hayo ambapo yeye binafsi alitoa Blanketi 300 na Turubai 200
kwa ajili ya wahanga hao kujisitiri.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi Msaada huo ,Balozi wa Kuwait ,Al Najeem amesema mbali na
msaada huo anataraji kuzungumza na Shirika la Huduma ya kwanza la nchini Kuwait
kuona namna ambavyo watashirikiana na Shirikiana na Shirika la Msalaba mwekundu
kusaidia wananchi hao.
Akitoa
taarifa ya athari ya Mafuriko hayo Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Senyamule
amesema wananchi wamekubalina kuhama kutoka eneo la Mafuriko ambalo wamekuwa wakifanya
shughuli za Kilimo na kupewa maeneo ambayo sasa watafanya makazi ya kudumu.
Waziri
wa Madini ,Angela Kairuki ambaye ni mwenyeji wa wilaya ya Same akatumia hadhara
hiyo kuwasilisha Pole kwa waathirika wa Mafuriko huku akipongeza serikali ya
mkoa na wilaya ya Same kupitia kamati za maafa kwa namna ambavyo wameweza
kushughulikia changamoto hiyo.
Waziri
Kairuki akawasilisha Ombi kwa wakazi wa kata ya Ruvu Marwa katika eneo la Kombo
kutumia vizuri msaada huo kutoka kwa wafadhili mbalimbali likiwemo Kanisa la
Kiinjili ka Kilutheli Tanzania (KKKT)
Zaidi ya watu wapatao7000 walilazimika kuyahama makazi yao baada
ya kufikwa mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zilizonyesha huku eneo
lililoathirika zaidi likiwa ni ukanda wa
tambarare wa wilaya ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.
No comments:
Post a Comment