Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao alipowasili katika kata ya Mshiri-Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo.(katikati) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira .
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao na viongozi wengine wa Dini wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa shughuli ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo katika Jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Vunjo wakati a uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo,uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri-Marangu.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri -Marangu .
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akizungumza jambo na viongozi wenzake wa Dini waliohudhuria mktano wa uzinduzi wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira akizungumza wakati wa mkutano huo .
Mmoja wa Viongozi wa Dini ya Kiislamu Sheakh ,Abdalah Mwacha akizungumza wakati wamkutano wa uzinduzi wa taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi zilizotolewa wakati wa Uzinduzi huo.
Diwani wa kata ya Mshiri,Exaud Mamuya akizungumza katika mkutano huo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia na Viongozi wengine kuelekea eneo ambalo uzinduzi wa Mitambo ya kukarabati barabara za jimbo la Vunjo ulifanyika.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akikata utepe katika mtambo unaotumika kukarabati barabara ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa Taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza barabara katika jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akibariki moja ya Mitambo itakayotumika katika kufanya matengenezo ya barabara katika jimbo la Vunjo.
Mtambo wa kukwangua barabara ukianza kazi muda mfupi baada ya kuzinduliw kwa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza miundo mbinu ya barabara.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini , Baba Askofu Dkt Martin Shao amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo itayoshughulika
na kutatua kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji.
Kwa kuanza taasisi hiyo imepanga kuanza matengenezo ya
barabara katika vijiji vyote Vilivyoko katika
Jimbo la Vunjo ,barabara ambazo zinakadiliwa kuwa na urefu wa Km 272.8 ambazo
zitagharimu kiasi cha Sh Bil 7 na Mil 290.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo
uliofanyika katika kata ya Mshiri ,Marangu wilaya ya Moshi ,Katibu wa Bodi ya
taasisi hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia amesema Vunjo
litakuwa jimbo la kwanza kufanya tukio hilo.
“Mzigo huu tulionao utakuwa mwepesi tukiw ana raha kwenye
nafsi zetu ,na tunataka tuongoze kama wana vunjo hili liwe jimbo la kwanza
Tanzania kwa watu wake kuwa na raha bila ya kuwa na bughdha za aina yoyote”alisema
Mbatia.
Alisema tukio la kuleta viongozi wa Dini pamoja ,viongozi wa
vyama vya siasa pamoja na ananchi pamoja kufanya na kukubaliana kwa maendeleo
yao na kwamba litakuwa ni jimbo la mfano kwa majimbo mengine kwa kuanzisha
utaratibu huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo,Askofu
Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Kaskazini Dkt Martin Shao alisema taasisi hiyo bado ni changa lakini hata hivyo
tayari imeweza kuanza kazi kwa upande wa miundombinu ya barabara.
“Hii taasisi yetu ni change kweli ,maana tarehe 23 mwezi Julai
ndio katiba yetu tumeiweka wazi mbele ya watu wote na ikapata Baraka za Mkuu
wetu wa mkoa wa Kilimanjaro,lakini leo mtoto huyu ambaye ana siku chache tu ameanza
kutembea na ameanza kufanya kazi”alisema Dkt Shao.
Kero za Muda mrefu sasa kwa wananchi katika jimbo la Vunjo
zikiwemo za Miundombinu ya barabara,Elimu,Afya na Maji sasa zitafika kikomo
huku suluhisho likitajwa kuwa ni kuanzishwa kwa taasisi hii ya Maendeleo
Endelevu katika jimbo la Vunjo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment