ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 20, 2018

Wabunge wa Kigoma wakutanishwa mradi wa pamoja na UN

 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kushoto) pamoja na Mchambuzi Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho wakipitia Programu ya Pamoja ya Kigoma na Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kwa mkutano uliohusisha Wabunge wa mkoa wa Kigoma na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (kulia) akifungua mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa (UN-KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha.
 Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini-CCM,  Daniel Nsanzugwanko akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa mkoa wa Kigoma wakati mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge hao juu ya mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kulia) akiwasilisha muhtasari wa mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma wakati wa mkutano maalum ulioandaliwa juu ya mradi huo wa pamoja uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini –CCM , Augustine Vuma akichangia maoni mara baada ya kupitishwa kwenye maeneo ya mradi wa pamoja wa Kigoma wa Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akifafanua jambo wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mbunge wa Jimbo la kigoma Kusini-CCM, Hasna Mwilima akichangia maoni yake katika eneo la muundo wa usimamizi katika Programu ya pamoja ya Kigoma na Umoja wa Mataifa mara baada ya kupokea muhtasari wakati wa wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mbunge wa jimbo la Buhingwe, Albert Obama akichangia maoni wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akifafanua jambo kwenye maeneo ambayo UNCDF yanahusika wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Faith Shayo (kulia) akielezea kuhusu mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UN Women pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) katika eneo la elimu wakati wa mkutano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani wa waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Kigoma kwa kushiriki mkutano maalum juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo na Wabunge hao ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Pichani ni Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa walioshiriki mkutano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Picha ya pamoja ya Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa na Wabunge hao ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi wetu
WABUNGE wa mkoa wa Kigoma walipata nafasi ya kutaarifiwa mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa ambao umejikita katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo na pia kutekeleza shughuli mbali mbali zinazolenga kufikia malengo endelevu ya dunia.
Akifungua mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliwataka washiriki wa mkutano huo kufuatilia kwa makini hatua iliyofikiwa ya mradi huo na kutoa mapendekezo yao.
Baadhi ya shughuli za mradi huo zimeanza kutekelezwa hususan katika maeneo ya Kilimo, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi, kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na kina mama pamoja na elimu.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waheshimiwa wabunge kutumia fursa waliyoipata kupokea taarifa kuhusu mradi na kutoa ushauri wa namna ya kufanikisha malengo yaliyowekwa ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma.
“Mkoa wa Kigoma ni Mkubwa na tunatamani kuona mradi huu unapanuka kujumuisha wilaya zote na pia sekta nyingine muhimu kama afya. “ alisema Maganga ambaye alisema kama serikali wako tayari kushirikiana na wadau wote wenye mapenzi na mkoa wa Kigoma wataliona hilo.
Katika mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez na wadau  wengine wa maendeleo, misingi imara ya ushirikiano kwa ufanikishaji wa maendeleo ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla yalizungumzwa na kuafikiwa.  
Mkuu huyo wa mkoa pia alimshukuru Bw. Alvaro, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Tanzania na waandaji wa kikao hicho.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa lengo kuu la kikao ni kujadiliana juu ya Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Mkoa wa Kigoma na pia kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mkoa huo. 
Kikao hicho cha wabunge kiliombwa kwenye Mkutano wa RCC wa mwaka jana na kutokana na kutokupatikana fursa kiliahirishwa mara kwa mara .
Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa Tanzania yanashirikiana na wadau wengine wa maendeleo na serikali kutekeleza mradi wa pamoja ambao utashughulikia masuala ya wenyeji na wakimbizi kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
“Shukrani za kipekee zimwendee Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa kamati ya uongozi ya mradi huu, Bw. Alvaro kwa mapenzi aliyo nayo kwa mkoa wa Kigoma hadi kuwa chachu ya uanzishwaji wa mradi huu. “ alisema Maganga
Naye Mratibu huyo  Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa wataendelea kuisaidia Tanzania kwa kutambua  umuhimu uliopo.
“Tanzania, na hasa Mkoa wa Kigoma, imepokea maelfu ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miongo mingi. Kitendo hiki cha ukarimu wa kuwapokea watu wanaoteseka, na kukimbia migogoro kinafanywa kwa niaba ya jumuiya ya kimataifa, nasi tunawapongeza sana kwa moyo huo,” alisema  na kuongeza kuwa changamoto kwa jamii ya wenyeji, kunalazimisha uwepo umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kujinusuru.
Kujinusuru, ndio chombo kikuu cha kinga kwa mkimbizi, na ni kigezo muhimu katika hatua za kiutu, ili kutoa mwitikio kwa mgogoro unaofukuta wa mahitaji ya kiutu.
Alisema kwamba UN wamegundua kwamba hakuna njia ya kuwahakikishia wakimbizi kinga kama mahitaji, maslahi na matamanio yao yataifanya jamii ya wenyeji kuchoka na kuibua mivutano kati ya jamii tofauti.
Alisema kuanzishwa kwa Mpango wa Pamoja wa Kigoma ni jitihada muhimu inayolenga kuunganisha mpango wa misaada ya kibinaadam, na ule wa kuleta maendeleo na kupunguza mzigo unaozielemea jamii za wenyeji.
Programu hiyo kwa sasa inaweka mkazo katika maeneo sita, yaani, nishati na mazingira endelevu; uwezeshaji kiuchumi vijana na wanawake; ukatili dhidi ya wanawake na watoto; elimu; maji, usafi na usafi binafsi (WASH); na, kilimo. Utekelezaji wa shughuli zilizo chini ya maeneo haya, unaendana na mipango ya sasa ya kitaifa na ngazi ya mkoa.

No comments: