Advertisements

Friday, August 10, 2018

KAMISHNA JENERALI PHAUSTINE KASIKE AAGANA NA MAOFISA MAGEREZA WANAOKWENDA NCHINI SHELISHELI KUTEKELEZA JUKUMU LA UREKEBISHAJI

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Mkaguzi wa Magereza Godfrey Mpagike(kulia) ambaye ni miongoni mwa maofisa na askari 20 wa Jeshi la Magereza ambao wanatarajia kuondoka Agosti 16, 2018 kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu kwa mkataba wa miaka miwili.
Maafisa wa Jeshi la Magereza ambao wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu kwa mkataba wa miaka miwili wakijadiliana jambo kama inavyoonekana katika picha mara baada ya kuagana rasmi na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuagananao leo Agosti 10, 2018 jijini Dar es Salaam. Maafisa hao wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza(walioketi) na askari wa Jeshi hilo vyeo mbalimbali(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya kuagananao leo Agosti 10, 2018 jijini Dar es Salaam. Jumla ya maafisa na askari 20 wa Jeshi la Magereza wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments: