Advertisements

Friday, August 3, 2018

MBUNGE VITI MAALUM (CCM), MKOA WA SINGIDA ATOA MSAADA WA MASHUKA KITUO CHA AFYA ILONGERO

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe (kushoto), akimkabidhi, Mganga wa Kituo cha Afya Ilongero, Grace Kishindo (katikati) mashuka 50, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kulia ni Mganga Msaidizi wa kituo hicho, Adamu Raphael Kito.
Mbunge Matembe, akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
Makabidhiano yakiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe ametoa msaada wa mashuka 50 kwa Kituo cha Afya cha Ilongero mkoani huko ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Matembe alisema yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na vituo vya afya mkoani humo.

"Mpaka sasa nimetoa msaada huo katika vituo viwili cha Ilongero na Kinyamburi na ninaendelea katika maeneo mengine" alisema Matembe.

Matembe alisema mbali ya kutembelea miradi hiyo pia anatembelea Jumuiya za Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) mkoani humo kuona jinsi zinavyoendelea kufanya kazi za kuimarisha chama.

(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990-0712727062)

No comments: