Advertisements

Sunday, August 5, 2018

Mwanamuziki Saidi Kanda & Mvula-Mandondo Band Kutingisha Onyesho la Tübingen, Ujerumani 2018

Ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Mvula-Mandondo Band yenye makao yake nchini Uingereza,inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe wa dansi mtanzania Saidi Jumanne Kanda aliyewahi kutamba na bendi za Super Matimila, na Bima Lee. mkongwe huyo wa muziki anakiongoza kikosi chake cha Mvula-Mandondo Band katika jukwaa kubwa la maonyesho ya kimataifa ya GaiExpo trade fair yanayoambatana intern.Afrika FestivalTübingen 2018 inchini
ujerumani ambalo mwaka huu "Focus country Tanzania". bendi ya Mvula-Mandondo Band itapanda jukwaani kuanzia siku ya Ijumaa ya 10 Agosti 2018 hadi Jumamosi 11 Agosti 2018 Maonyesho hayo yanawashirikisha na wajasilimali ,wafanyi biashara,wasanii na wanamuziki na kuwakusanya umati watu zaidi ya laki moja katika viwanja vya Fest-Platz,mjini Tübingen,kusini mwa ujerumani.bendi ya Mvula-Mando inatarajia kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa nchini ufaransa mwezi Septemba.usikose kujumuika na waadaau wengine katika maonyesho haya makubwa ambapo wasanii na wajasilia mali toka Tanzania wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya "Hapa Kazi Tu"

No comments: