Advertisements

Monday, August 6, 2018

UN yakabidhi mipira Yes Tanzania kufundishia SDGs

Pichani juu na chini ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (kulia) mipira itakayotumika kufunza vijana kuhusu SDGs na wajibu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (katikati) akimkabidhi Necta Mussa (kulia) kijana ambaye aliwakilisha wenzake mipira itakayotumika kufunza vijana hao kuhusu SDGs na wajibu wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea mipira hiyo ya kuhamasisha vijana kuhusu SDGs na wajibu kupitia michezo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa vijana kutoka YES Necta Mussa na kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi mipira yenye chapisho la SDGs kwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya (kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa vijana kutoka YES Necta Mussa (kulia) akitoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa mara baada ya kupokea mipira hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES, Kenneth Simbaya wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Na mwandishi wetu

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez amewataka vijana kutoka ndani walikojificha ambako wanatumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na kwenda nje kushirikiana katika kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) yanafanikiwa.

Mratibu huyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo (UNDP) alisema hayo wakati alipokuwa akikabidhi mipira kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya YES itakayotumika kufunza vijana kuhusu SDGs na wajibu.

Yes Tanzania ni taasisi ya vijana inayojishughulisha na kuelimisha vijana kupitia michezo na ina makao makuu yake Mbeya.

Rodriguez alisema kwamba vijana ni lazima wawajibike katika kuhakikisha kwamba wanajihusisha na maendeleo ya taifa kwa kushirikiana katika kujifunza na kuongozana kuhakikisha dhima ya dunia kuwa mbele kimaendeleo ifikapo mwaka 2030 inafikiwa.

Alisema mipira iliyokabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa YES, Kenneth Simbaya ambayo ina chapisho la SDGs imetolewa ili kusaidia kufikisha ujumbe kwa vijana wa kuachana na mawasiliano ya upweke katika mitandao na kujituma kwa pamoja kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Ni mategemeo ya mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa, mipira hiyo itatumika kuwaweka pamoja vijana kujadiliana kuhusiana hatima yao na utekelezaji wa malengo ya maendeleo.

Akipokea mipira hiyo Simbaya wa YES alisema kwamba taasisi yake inayohusisha na vijana hutumia michezo kutoa elimu na kwamba mipira hiyo itatumika kusambaza malengo hayo ya dunia kwa vijana vijijini.

Simbaya alisema kwamba kwa sasa malengo hayo yanajulikana vyema mijini lakini vijijini ni bado kwa hiyo watatumia mipira hiyo kufikisha elimu na ushawishi miongoni mwa makundi ya vijana kupitia michezo.

Alisema wao wanaamini kwamba kwa kuwezesha vijana unaliweka taifa katika mazingira mazuri yanayoeleweka kwa ajili ya huduma miaka ijayo.

Alisema anaamini kwamba maendeleo ya vijana na SDGs hayawezi kutengana kwani ni dira sahihi katika kufanikisha hali ya baadaye ya taifa.

Naye Necta Mussa kijana ambaye aliwakilisha wenzake katika kupokea mipira hiyo alisema kwamba wanaishukuru UN kwa kuwasaidia mipira hiyo ambayo wataitumia si tu kuwasiliana bali kutengeneza uwezo na afya njema kwa ajili ya ushiriki wa gurudumu la maendeleo.

Alisema michezo inajenga kujiamini na kufungua milango ya uongozi hivyo kwa kupata mipira hiyo kunawafanya vijana kuwa pamoja na hivyo kushirikishana katika kutengeneza uwezo wa kujiletea afya na maendeleo ya kiuchumi.

No comments: