ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 13, 2018

SERIKALI KUPELEKA WATAALAMU WA UTAFITI WA MIAMBA(GST),MALIASILI NA MAZINGIRA AMANI MUHEZA



NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani

NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo  wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa ziara yake ya siku moja

NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayanu humo
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akisistiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo

Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sakale katika kata Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza wakati wa ziara ya Naibu
Waziri wa Madini Dotto Biteko juzi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo

SERIKALI imesema kuwa itafanya mchakato wa kuleta wataalamu wa utafiti wa miamba(GST),maliasili na mazingira kwa pamoja katika kata ya Mbomole tarafa ya Amani ili kuweza kuona uwezekano wa kuwaruhusu wananchi na wachimbaji wadogowadogo kuchimba madini katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika kata hiyo wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na ni mengi yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

Walisema kuwa kutoka uliopo mwamba unaosadikiwa kuwa na madini na chanzo cha maji ni zaidi ya mita sitini na ilipo hifadhi ya msitu wa asili wa Amani ni zaidi ya mita 3,000 lakini wamekuwa wavumilivu kusubiri hatima ya serikali.

“Mheshimiwa naibu waziri uchumi tunao lakini tunakufa maskini…hapa madini yapo lakini serikali imetuzuia kwa hatari ya uharibifu wa mazingira ..sisi tunakuhakikishia hakuna uharibifu wowote wa mazingira utakaotokea” alisema Shetwai

Naye diwani wa kata hiyo Anord Mlowe alisema kuwa wataalamu walikuja kupima mwamba na baadae ukaanza kutoa madini lakini baadae kukaanza mabishano kati ya watu wa maliasili,maji na mazingira kuhusu usafishaji wa madini kwa kutumia zebaki lakini mkuu wa wilaya ya Muheza aliyepita Subira Mgalu alijiridhisha kuwa hakuna madhara lakini serikali ikaweka zuio.

Alimuomba wziri kuwaruhusu ili waweze kuchimba kutoka maeneo yalipo mmwamaba wa madini ni mashamba ya wananchi na sio eneo la hifadhi kutokana wameyarithi kutoka kwa mababu zao.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Muheza balozi Adadi Rajabu alimuomba naibu waziri Biteko kuleta wataalamu wa madini kuja kupima ili kuona kama madini hayo yanatoka milimani au yapo kwenye mto ili kuona namna ya kuwasaidia kupewa eneo la uchimbaji.

“Mheshimiwa naibu waziri pale mwamba uko pembeni kutoka chanzo cha maji na wananchi wa Sakale kata ya Mbomole wametunza msitu wa asili wa Amani….hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kutunza msitu bila ya kuathiri chanzo cha maji” alisema.

Aliongeza “kwa niaba yao tuma wataalamu wako waje ili wakuletee taarifa ili wananchi hawa waweze kuchimba”.

Kwa upande wake naibu waziri Biteko alisema kuwa kiu ya serikali ni kuwapatia maeneo ya uchimbaji wachimbaji wadogowadogo ili waweze kubadilisha maisha yao kupitia uchumi wa madini hii ni kutokana Rais kubadilisha sheria za nchi kwa upande wa madini kutoka kuwanufaisha wageni na sasa kuwanufaisha watanzania.

“Serikali yenu ni sikivu,mheshimiwa Rais amebadilisha sheria ya madini ili kuwanufaisha watanzania badala ya wageni ,hapa leo tumekuja kuangalia kwa macho ili tufanye uamuzi sahihi …siwezi kumiambia mchimbe sasa hivi ila tutaleta wataalamu wetu wa GST,maliasili na mazingira kwa pamoja ili waje kuona uwezekano wa kupewa eneo la kuchimba ikiwa hapa au kwengine”alisema.

Aidha aliongeza kuwa wananchi lazima wafundishwe kufuata sheria za madini haswa katika kuhama matumizi ya zebaki katika kuchenjua madini ambayo yana athari kubwa kwenye mazingira na miili ya binadamu kutumia madini ya Sayayi ambayo hayana madhara. Awali mkuu wa wilaya ya Muheza mhandisi Mwanaasha Tumbo akisoma taarifa ya zuio la uchimbaji wa madini eneo hilo, alisema lengo ni kulinda mazingira na chanzo cha maji licha ya sheria katika maeneo hayo matatu ya madini,mazingira na maliasili kukinzana jambo ambalo linaleta ugumu kwa watendaji kuwadhibiti wachimbaji hao.

No comments: