ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 12, 2018

WAZIRI LUGOLA AENDA KUHANI MSIBA NYUMBANI KWA MWANAHABARI MAREHEMU SAGATI, MWIBARA WILAYANI BUNDA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, katika Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Waziri Lugola alifika msibani ili kutoa pole kwa wafiwa kijijini hapo, leo Jumamosi Agosti 11, 2018. Wapili kutoka kulia ni Mfungo Sagati, baba wa marehemu, na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akimpa mkono wa pole Mfungo Sagati, baba wa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, mara baada ya Waziri huyo kufika cha Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara kwa ajili ya kutoa pole kwa familia
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na Dora Mwishangi (kushoto), mama mdogo wa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, katika Kijiji cha Mwiruruma, Kata ya Iramba, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, leo Jumamosi Agosti 11, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (katikati) akisaini kitabu cha maombolezo, alipofika nyumbani kwa Mwanahabari marehemu Shadrack Sagati, aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Geita Julai 31, 2018. Kushoto ni Mfungo Sagati, baba mzazi wa marehemu, na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaka Mahera.

No comments: