Advertisements

Sunday, August 5, 2018

WAZIRI MHAGAMA AHIMIZA UZALISHAJI ZAIDI OFISI YA MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na watumishi wa ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, alipofanya ziara ofisini hapo Agosti 4, 2018 Jijini Dodoma. (Kushoto) Kaimu Mpiga Chapa Mkuuwa Serikali Bw. Hyacinth Komba, Kaimu Afisa Mfawidhi Bw. Silver Chindandi na Mpiga Chapa Bw. Prosper Chokala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia jalada ambalo limetengenezwa na kiwanda cha uchapaji kilichopo ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali alipofanya ziara fupi ofisini hapo Jijini Dodoma, Agosti 4, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza kwa makini maelezo ya Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali alipotembelea ofisi hiyo kukagua uendeshaji wa kiwanda hicho agosti 4, 2018 Jijini Dodoma.
Afisa Mfawidhi Bw. Silver Chindandi kimwelezea jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanaya ziara fupi ofisini hapo kujionea shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho, Agosti 4, 2018 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

NA MWANDISHI WETU:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama awataka watumishi ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuongeza bidii ya uzalishaji na kuwa wabunifu katika kutafuta masoko zaidi nchini.

Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili kukagua shughuli za uendeshaji wa kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali jijini Dodoma, Agosti 4, 2018.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo aliwasisitiza watumishi wa ofisi hiyo kuwa wabunifu kwa kutumia vifaa walivyonavyo ili kuongeza uzalishaji na kutafuta masoko zaidi nchini yatakayowasaidia kupata mapato zaidi ya kuendeshea shughuli za kiwanda hicho.

“Ni vyema mkatumia fursa ya taasisi na mashirika yaliyopo nchini kutafuta masoko ya kutengeneza majalada yao. Mfano tunao mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao utahitaji kutoa majalada mengi kwa ajili ya kuelimisha umma juu ya majukumu yao. Hivyo ni vyema mkawa wabunifu kwa kuongeza bidii katika kutafuta masoko zaidi kwenye Mawizara, Taasisi na Makampuni yaliyopo nchini.” alisisitiza Mhagama

Kwa upande wake Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Hyacinth Komba alieleza kuwa watafuata maagizo ya waziri kwa kuboresha shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho na kuahidi kutekeleza majukumu yao.

Aidha, aliomba Serikali iwawezeshe kwa kuwaongezea vifaa na mitambo ili waweze kuongeza uzalishaji zaidi.

No comments: