ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 28, 2018

SERIKALI YATUMIA BILIONI 5.6 KUIWEZESHA TAASISI YA MOI KUWA NA MRI,CT SCAN, X- RAY NA ULTRA SOUND

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata maelezo ya hatua iliyofikiwa katika usimikaji wa mashine ya CT Scan, wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt Respicious Boniface pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja ya machine mpya ya X-ray ya kisasa ambayo iko tayari kutumika. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface.
Mtaalamu wa viungo bandia wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Deus David akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusu namna viungo bandia vinavyotengenezwa na kufanya kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na moja ya mgonjwa ambaye anatengenezewa kiungo bandia MOI ili kubainisha changamoto zilizopo zinazomkabili mgonjwa huyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile Dkt Ndugulile akimjulia hali mtoto anayepata Huduma katika Taasisi ya MOI.(PICHA ZOTE NA MOI)

1 comment:

Tumaini Geofrey Temu said...

waganga wa jadi deal hamna kitu hapo kizunguungu cha wazungu