Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya Mfalme wa Ubelgiji yaliyofanyika katika makazi ya Balozi wa Ubelgiji jijini Dar Es Salaam jana. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya.
Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter van Acker akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mfalme wa Ubelgiji yaliyofanyika katika makazi yake jana.
Dkt. Ndumbaro akiendelea kuhutubia.
Dkt. Ndumbaro akigonganisha glasi na Balozi Peter van Acker kwa kuwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli na Mfalme wa Ubelgiji
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb.) wa kwanza kulia akizungumza na Meneja wa mauzo wa Kimataifa wa kampuni ya Cardolite kutoka Ubelgiji Bw. Hans Carleer pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Mohamed Kamal (wa kwanza kushoto).
Kampuni
32 kutoka Ubelgiji zilizowekeza Tanzania ni chache ukilinganisha na
uwingi wa fursa za uwekezaji zilizopo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa
bado hazijatumika kikamilifu.
Kauli
hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) katika hafla ya kuadhimisha
Siku ya Mfalme wa Ubelgiji iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi jijini
Dar Es Salaam tarehe 16 Oktoba 2018.
“Tanzania
ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali kama vile;
kilimo, ujenzi wa miundombinu, nishati, madini, teknolojia ya habari na
mwasiliano, afya, viwanda vya uzalishaji, mafuta na gesi ambazo
hazijatumika ipasavyo. Hivyo, Ubelgiji na Tanzania zikijizatiti zinaweza
zikafanya biashara na kufanya uwekezaji mkubwa na wenye manufaa kwa
pande zote mbili), Dkt. Ndumbaro alisema.
Alielezea
matumaini yake kuwa ujio wa Makampuni makubwa ya Ubelgiji zaidi ya 40
ambayo yamekuwa na mazungumzo yenye tija na Makampuni ya Tanzania na
sekta nyingine zinazohusika na uwekezaji kwa siku tatu zilizopita,
utaleta ongezeko la uwekezaji na kuimarika kwa kiwango cha biashara kati
ya Ubelgiji na Tanzania.
Kwa
upande wa biashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Mhe. Naibu Waziri
ameridhishwa na urari wa biashara uliopo, ingawa alisisitiza umuhimu wa
kuimarisha zaidi. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, biashara kati ya
Ubelgiji na Tanzania imefikia kiwango cha Dola milioni 332 huku Tanzania
ikiuza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 208 nchini Ubelgiji.
Dkt.
Ndumbaro alihitimisha hotuba yake kwa kuishukuru Ubelgiji kwa kuendelea
kuwa mshirika mkubwa wa jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
Alitoa mfano wa programu mbalimbali za maendeleo nchini zinazoghramiwa
na Serikali ya Ubelgiji kwa kiasi cha Euro milioni 20.
Program
hizo zinajumuisha upatikanaji wa maji safi vijijini na uendelezaji
endelevu wa sekta ya kilimo katika mkoa wa Kigoma. Utekelezaji wa miradi
hiyo imesaidia kuboresha usimamizi mzuri wa vyanzo vya maji, usimamizi
wa rasilimali na mnyoro wa thamani katika kilimo, hususan kwa wakulima
wadogo.
Kwa
upande wake, Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Peter van Acker
alisema kuwa Ubelgiji itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya
awamu ya tano za kubadalisha maisha ya watu masiikini. Alisema jitihada
hizo pamoja na mambo mengine, zitaeendelea kuunga mkono juhudi za
Tanzania za kuleta utulivu wa kisiasa katika eneo la maziwa makuu
ikiwemo usuluhishi wa mgogoro wa Burundi.
No comments:
Post a Comment