ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 7, 2018

NAIBU BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. DAVID EYAL ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)

Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongea na wazazi wa watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.

NA GENOFEVA MATEMU – JKCI
ZAIDI ya watoto 750 wenye matatizo ya moyo hapa nchini wamefaidika na matibabu ya moyo kutoka kwa wataalam wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart - SACH) la nchini Israel tangu mwaka 1999.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. David Eyal alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa kutoka SACH kwa kushirikiana na JKCI.
Mhe. Naibu Balozi Eyal alisema watoto hao kutoka Tanzania Bara na Visiwani walifanyiwa uchunguzi na kutibiwa hapa nchini wale ambao walikutwa na matatizo yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu walipelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu zaidi. Gharama za usafiri na matibabu ziligharamiwa na Serikali ya Israel.
“Kujitoa kwa wataalam kutoka Shirika la SACH kuja Tanzania kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni ubalozi wa kweli wa kuitangaza nchi ya Israel kwa vitendo, ni matarajio yetu kuwa huduma hii itakuwa endelevu na kuendelea kuokoa maisha ya watoto wetu wengi zaidi”, alisema Mhe. Naibu Balozi Eyal.Alisema Israel itaendelea kushirikiana na JKCI katika mambo mbalimbali ikiwemo kutoa matibabu ya kina kwa watoto na kutoa udhamini wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema wataalamu kutoka Israel wanafika katika Taasisi hiyo mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto. Kuwepo kwa kambi hizo za matibabu ya pamoja kumewaongezea ujuzi madaktari, wauguzi, wataalam wa usingizi na mashine za moyo.

“Hivi sasa tuna kambi maalum ya siku sita ya uchunguzi na matibabu kati ya madaktari wetu bingwa wa moyo kwa watoto kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart - SACH) la nchini Israel. Licha ya kutoa huduma ya matibabu kuwepo kwa kambi hii pia ni njia mojawapo ya kuimarisha mahusiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na Israel”, alisema Prof. Janabi ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo. Jumla ya wataalamu 32 ambao ni madaktari, wauguzi na wataalamu wa mashine za moyo kutoka Israel wanashiriki katika kambi hiyo ya matibabu ya moyo ambapo watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongozana na mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akielekea kuangalia ukarabati wa jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI.
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiangalia kipimo kinachoonyesha jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto(Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI.
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) ambaye ni daktari bingwa wa wagonjwa mahututi Vivienne Mlawi alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David pamoja na wafanyakazi wengine na JKCI na Israel wakimuombea Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Marehemu Onesmo Mhewa aliyefariki mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David pamoja na wafanyakazi wengine wa JKCI na Israel mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa moyo wa mtoto Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKC.
Mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akimweleza Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David jinsi ukarabati wa jengo la watoto unavyoendelea. Mhe. David alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI.(PICHA NA ANNA NKINDA – JKCI

No comments: