Advertisements

Friday, November 16, 2018

SAYONARA PARTY NAHA OKINAWA, JAPAN

Meza kuu magwiji wa karate ngazi ya juu kabisa wa Jundokan So Honbu.Masters:

Kancho Yoshihiro Miyazato mwenyekiti wa Jundokan pia ni mtoto wa Eiichi Miyazato, Yasuda sensei, Kinjo sensei, Gima sensei, Higa sensei, Nakada sensei(USA), Renee sensei(France), Merriman sensei(USA) na Gsodam sensei ( Austria).
Meitatsu Yagi kulia wa Meibukan Goju Ryu ni mtoto wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chojun Miyagi sensei, Meitoku Yagi mwanzilishi wa Meibukan Goju Ryu, kati ni master wa Okinawa Kobudo.
Master Tetnosuke Yasuda Dan 10, umri wa zaidi miaka 94 na sensei Fundi Rumadha, Asato Royal Orion Hotel
Mwenyekiti wa Jundokan ambae pia ni mtoto wa mwanzilishi wa chama hicho master Eiichi Miyazato, pia ndie aliyekuwa mwalimu wa sensei Bomani mwanzilishi wa tawi la Jundokan Tanzania 1973.
Katika ufungaji wa sherehe hizo, pia walitunukiwa shahada au Dan wale wote walio pita mitihani yao asubuhi kabla ya sherehe. Ngazi ya juu kabisa katika shere hii kutunukiwa Dan, ni "master" Rony Kluger toka Israel aliyefuzu na kupewa shahada ya dan ya 9 na kuwa na cheo cha "Hanshi". picha juu akifanya kata ya Tensho.

No comments: