Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akizungumza na walimu pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda akizungumzia mchakato uliopitiwa mpaka kuwapa washindi wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni ‘Mentor’ wa Raymond Luanda kutoka Nlab Innovation Academy, Bw. Wilhelm Oddo, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Lumumba ya Visiwani Zanzibar, Bw. Ami Vuai, Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo pamoja na Mkutubi Mkuu wa Maktaba ya Kuu ya Taifa, Baraka Mcharazo akimwakilisha Mkuu Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Dr. Alli Mcharazo.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Msimbazi ambaye pia ni Mwalimu wa Elimu maalum wa shule ya walemavu Kimanga Sekondari , Bi. Sylvia Ruambo akielezea furaha yake baada ya kupokea tuzo wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Lumumba ya Visiwani Zanzibar, Bw. Ami Vuai akitoa neno la shukrani wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu aliyefanya vyema katika utoaji wa huduma za elimu, Bi. Sylvia Ruambo (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda
Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu aliyewezesha changamoto kuondolewa katika utoaji wa huduma za elimu kutoka Visiwani Zanzibar, Bw. Ami Vuai (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda
Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu wa mfano katika utoaji wa huduma za elimu nchini, Bw. John Bosco (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda.
Sehemu ya walimu na wageni waalikwa walioshiriki hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na HIMT AWARDS na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda.
Mgeni rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu walioshinda tuzo pamoja na wawakilishi wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na wageni waalikwa pamoja na walimu waliokabidhiwa tuzo wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na Wakufunzi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam (kushoto) pamoja na Queen Mtega (kulia) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu,
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limewataka walimu nchini kuendeleza juhudi wanazozionyesha katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili kuendelea kuinua kiwango cha elimu kinachotolewa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Elimu kutoka UNESCO, Faith Shayo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali kwa walimu na wadau iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha ‘America Corner’ uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutambua michango mbalimbali ya walimu hao katika ufundishaji na maeneo mengine ambayo kimsingi yanaleta tija katika kukuza maendeleo ya Taifa.
Alisema licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, walimu nchini wamekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao, suala alilowataka kutokufa moyo na badala yake kuongeza bidii.
“Sote tunashuhudia namna ambavyo walimu wanavyojitahidi kutimiza wajibu hao kikamilifu kila siku licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu katika kuinua maendeleo ya Taifa” alisema Faith.
Alisema tuzo hizo zinapaswa kuchukuliwa kama changamoto na walimu hao kwa kufanya vizuri wakati wote wanapotimiza wajibu wao wa kazi, hatua ambayo pamoja na sababu mengine zitawafanya wazidi kupata mafanikio.
Aidha alimpongeza muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda kwa kubuni wazo hilo lililolenga kutambua mchango wa walimu nchini, suala alilosema kuwa kwa kiasi kikubwa litazidi kuwapa moyo wa kazi walimu hao.
Awali muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda, alisema ‘How is My Teacher’ ni wazo alilolibuni kwa ajili ya kutambua mchango unaotolewa na walimu wote hapa nchini ikiwa na lengo la kuwahamasisha kuongeza msukumo katika utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji.
Alisema tuzo hizo ambazo ni mara ya kwanza mwaka huu, zinatarajiwa kuwa endelevu kila mwaka kwa lengo la kuendeleza utamaduni wa kutambua mchango wa walimu hao.
Jumla ya tuzo kumi zilitolewa kwa walimu mbalimbali waliopatikana kupitia mchakato maalumu wa uliowahusisha wanafunzi kupendekeza walimu wao na baadae kupigiwa kura.
No comments:
Post a Comment