Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) .
Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati wa uzinduzi ya kuchanga ujenzi wa Miundombinu ikiwemo Hosteli katika chuo hicho.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MoCU) Prof,Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katik aukumbi wa mikutano wa Ushirika .
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Miundombinu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Noel Nko ambaye pia ni mhitimu wa chuo hicho akizungumza juu ya wazo la kuwashirikisha Wahitimu wote wa Chuo hicho tangu mwaka 1963 katika kuchangia ujenzi wa miundombinu Chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof ,Faustine Bee akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira alipotembelea baadhi ya maeneo katika Chuo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu katika chuo hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wanaoishi
katika hosteli za nje ya chuo hicho wako kwenye mazingira hatarishi kutokana na
baadhi yao kufanyiwa vitendo vya kinyama huku ikidaiwa wengine tayari
wamepoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.
Matukio mengine yanayotajwa kuwafika Wanafunzi hao ni pamoja
na kuvamiwa na kuporwa mali ,kujeruhiwa kwa kuchomwa visu na kupigwa hasa kwa
wanafunzi wa jinsia ya Kike jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limechangia baadhi
yao kuathirika kimasomo na hata kupunguza hali ya kuendelea na masomo.
Kutokana na hali hiyo, Wahitimu wa Chuo hicho kuanzia mwaka
1963 wameanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli yenye
uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 ili kupunguza changamoto zilizopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Harambee hiyo Mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira amesema miundombinu ya Chuo kikuu cha Ushirika
Moshi haikidhi mahitaji ya sasa na ya baadae kwa wanafunzi wa elimu ya juu na
kwamba kwa kiasi kikubwa inahitaji kuboreshwa.
Dkt Mghwira amesema hosteli zilizopo sasa zilizojengwa miaka
ya 60 na 70 , pamoja na kuwa katika hali ya uchakavu zinauwezo wa kuchukua
wanafunzi 766 tu ikiwa ni sawa na asilimia 20 ya idadi ya wanafunzi waliopo na
ambayo inaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka .
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika
,Moshi (MoCU) Prof ,Faustine Bee alisema jambo ambalo limeibuliwa na wahitimu
wa chuo hicho ni jema na kwamba Uongozi wa chuo utaendelea kuwaonga mkono
katika jitihada hizo.
“Niwashukuru kwa kuja na wazo hili ,nimpongeze Noel Nko
ambaye amejitolea kuwaongoza wenzake katika jambo hili,sisi kama viongozi na
wadau tunawashukuru na tunawaunga mkono kaitka jitihada hizi,mchango wao ni
mkubwa na unachangia katika kuunga mkono juhudi za rais Magufuli ya kuona
taasisi za elimu zinakuwa na mundombinu iliyobora”alisema Prof Bee .
Alisema uwepo wa miundombinu bora kutatoa nafasi kwa
wanafunzi kujifunza kwa bidii huku akiishukuru Serikali kwa kutoa kiasi
cha Sh Bil 1.3 ambazo tayari zimesaidia katika kuboresha baadhi ya miundombinu
ya chuo hicho.
“Hata hivyo bado hatujakamilisha ,tunamahitaji mengine
makubwa kama barabara za ndani hazijakamilika,tumefanya tu sehemu ,lakini pia
upande wa malazi kwa wanafunzi ni changamoto ,wanafunzi wetu kiasi cha silimia
70 wanakaa nje ya chuo na kati ya hao kuna vijana wa kike ambao wanahitaji
uangalizi mkubwa”alisema Prof Bee.
Naye Mwenyekiti wa Harambee hiyo,Noel Nko alisema wakati huu
chuo kikiendelea kukua tuliona ni vyema wanafunzi wote waliohitimu chuoni hapa
tangu mwaka 1963 tuone ni kitu gani tunaweza tukafanya kwa chuo zikiwa ni moja
wapo ya kuunga mkono serikali.
“Niombe kutoa hamasa kwa wahitimu wote wa Chuo Kikuu cha
Ushirika zoezi hili tulifanye kwa moyo ,hamasa itakuwa kwa mwenye kiasi
chochote cha fedha atachangia na harambee hii itakuwa endelevu ,tutaifanya wanaushirika
nchi nzima na niwaombe wanaushirika kote nchini ,wakiwa ni warajisi wa
mikoa,maafisa ushirika wa halmashauri,popote pale walipo wahamasihe zoezi hili
kwa nguvu zote”alisema Nko.
Kukamalika kwa harambee hii kwa kiasi kikubwa litasaidia
kuboresha ulinzi na usalama kwa wanafunzi pamoja na mali zao sambamba na
kuboresha mazingira ya kujifunzia na kujisomea kwa wanafunzi na pia itasaidia
wanafunzi wengi wa kike kupata elimu bora .
Mwisho
No comments:
Post a Comment