Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akimkabidhi zawadi ya vitabu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mtwara Titus Mdoe
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akimkabidhi zawadi ya vitabu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akitoa hotuba siku ya mkutano wa amani ulifanyika katika viwanja wa MAsjid Batul Karim Mkoani Mtwara.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa na baadhi ya waumini wa dini hiyo katika uzinduzi wa radio ahmadiyya .mh mkuu wa mkoa alikuwa mtu wa kwqanza kusaini kitabu cha wageni .
Kupitia mkutano wa Amani ambao umeandaliwa na waislamu na jumuiya ya waislam Ahmadiyya mkutano ambao uliwakutanisha viongozi wa asasi sizizo za kiserikali,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa serikal mkutano ambao ulifanyika siku ya ijumaa tarehe 21/12/2018. Mgeni maalumu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa ameipongeza Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya kwa kufanya mkutano wa amani ikiwa ishara tosha kabisa kuelezea islamu na amani amendelea kuwasisitiza viongoz wa dini kuwakumbusha waumini swala la amani.
Pia katika mkutano huo mkuu wa mkoa alifungua rasmi kituo cha kurushia matangazo cha radio ahmadiyya 99.3 mHz ambacho kwa sasa kinasikika ndani ya manispaa ya mtwara mikindani na kuwataka wanahabari kufanya kazi kwa weledi na uadilifu na kushirikiana na serikali ufahasa kupitia redio huku akiendelea kusisitiza watu kuienzi amani.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Ahmadiyya kwa kuenzi amani na kuiga kutoka kwao kwa kufanya mikutano kama hii mara kwa mara na kutoa pongezi kwa jumuiya kwa kutoa mafundisho ya utii wa serikali pia ametahadharisha wote ambao watakaovunja amani kwa kisingizio cha dini watashughulikiwa kama wahalifu.
No comments:
Post a Comment