Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitazama ubadilishaji wa hotuba za Mwalimu Nyerere kutoka kwenye Analogi kwenda Digitali wakati alipotembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) mitambo ya makumbusho iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) meza iliyotumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya mahojiano iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo
tarehe 21 Disemba 2018 ametembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika iliyozinduliwa miezi mitano iliyopita na Shirika
la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere
jijini Dar es salaam.
Mhe Hasunga ametembelea Studio hiyo yenye
kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika
kanda za sauti na video ikiwa imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na
Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha
Dachi, amemueleza Waziri wa kilimo kuwa Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga
kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti
ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.
Alisema kuwa Studio hiyo ni sehemu ya mradi
mkubwa wa hifadhi ya mambo ya urithi (TAHAP) wenye lengo la kuhamasisha hifadhi
na utunzaji wa urithi wa Tanzania na kumbukumbu za mapambano ya ukombozi katika
bara la Afrika, pia itaongeza uelewa wa watanzania juu ya urithi wao ambao
umekuwa ukiongezeka jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele.
Akizungumza mara baada ya kutembelea studio
hizo, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amelipongeza Shirika la
utangazaji la Taifa-TBC kwa kuwa na eneo hilo muhimu kwa ajili ya kuhifadhi
kumbukumbu mbalimbali ili kuhakikisha kuwa urithi wan chi unahifadhiwa kwa
manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mhe Hasunga amesema kuwa kuweo kwa studio hiyo
itaongeza ufanisi wa kuhifadhi kumbukumbu za maandishi, sauti n ahata video
katika weledi na ufanisi mzuri.
UNESCO kwa kushirikiana na Wadau na Washirika wa Mradi wa Umoja wa Ulaya (EU); kwa ufadhili wa Mradi wa Uhifadhi na Uendelezaji wa Hifadhi za Urithi Tanzania, hususani Hifadhi ya Urithi wa Kiafrika, kwa pamoja walizindua Studio za Mwalimu Nyerere – zijulikanazo kama Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika Ijumaa tarehe 27 Julai 2018.
Mhe
Hasunga amesisitiza kuwa Studio hiyo ni tunu muhimu ya urithi na eneo la kihistoria
ambalo lilitumiwa sana katika zama za Ukombozi kama kituo cha utangazaji kikiwa
na huduma za mifumoya nje iliyowekwa mahususi kwa Harakati za Ukombozi wa
Kusini mwa Afrika.
TBC (iliyojulikana
kama Radio Tanzania) ilirusha hewani vipindi na kuajili waandishi wa habari
kutoka karibu maeneo yote yaliyokuwa na harakati za ukombozi.
No comments:
Post a Comment