ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 3, 2019

Idara ya ustawi wa Jamii yatakiwa kuandaa haraka sera ya Wazee

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Idara ya Ustawi wa Jamii kuhakisha inandaa haraka sana Sera ya Wazee kwa kuwa sera iliyopo ni ya siku nyingi na ilianza tangu mwaka 2003 hivyo inatakiwa sera mpya itakayoendana mabadiliko ya sasa.

Dkt Ndugulile amesema hayo wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya wazee nchini.

Naibu huyo ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuarakisha mchakato wa kukamilisha mapema mswada wa sheria ya wazee wa nchini ili haki na stahili za wazee zisiwe suala la hiari bali ziweze kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Dkt. Ndugulile pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 29 Januari Mwaka huu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Ustawi wa Jamii kukamilisha mapema sheria ya masuala ya ustawi wa jamii Nchini ili ofisi yake iweze kutoa mrejesho kwa ofisi ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa suala hilo.

Pia Dkt. Ndugulile pia ameagiza sambamba na utekelezaji huo pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuharakisha maandalizi ya muundo wa kada ya ustawi wa jamii ambao utaainisha madaraja, kazi na nini watapaswa kufanya suala ambalo pia ni agizo la Waziri Mkuu.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika maandalizi mapya ya Sera ya Afya nchini suala la wazee limepewa kipaumbele kwa kuzingatia masuala ya tiba kwa wazee na kwa mala ya kwanza Wizara imetambua sayansi ya tiba ya wazee na imetamkwa wazi katika sera ya Afya kwa mantiki hiyo katika Wizara ya Afya kutakuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya tiba na afya za wazee.

No comments: