Advertisements

Saturday, February 9, 2019

WATEJA SITA BENKI YA NMB WAJINYAKULIA SIMU KALI KATIKA PROMOSHENI YA MASTA BATA

Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza wakati wa Promosheni ya washindi wa droo ya nane ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBatan iliyofanyika katika Tawi la Benki hiyo la Sinza Mori jijini Dar es Salaa. Kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki hiyo la Sinza Mori, Mnkande Zawadi.
Tabitha Luhuja wa Benki ya NMB (wa pili kulia), akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya nane ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata. Kutoka kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori, Mnkande Zawadi, Sophia Mwamwita, Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemedy na Bi. Saumu Rajabu kutoka Selcom.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo, Yusuph Achayo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu promosheni hiyo.

Na Mwandishi Wetu

WATEJA sita wa Benki ya NMB wamejishindia simu janja 'Samsung S9+' baada ya kuchezeshwa droo ya nane ya shindano la Benki hiyo ya kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Washindi hao wapya wanakamilisha idadi ya washindi 12 hadi sasa waliojishindia simu kama hizo katika shindano hilo.

Washindi walioshinda na kujinyakulia simu hizo wametajwa kuwa ni Taha Karimjee kutoka maeneo ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, Gladys Gilbert, Salim Abdallah, Raphael Schuurmans wa Masaki jijini Dar es Salaam, Imara Noah wa Meatu na Burton Anyisile wa Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumzia kuhusu promosheni hiyo Meneja wa Benki hiyo Tawi la Sinza Mori, Mnkande Zawadi alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi za simu hizo.

Alisema katika droo ya mwisho washindi watatu watapata ofa ya kwenda kula 'Bata' Dubai huku wakiambataba na mtu mmoja wa kila mshindi ambapo jumla yao watakuwa sita na gharama zote za safari hiyo zitalipwa na benki hiyo kwa siku nne watakazo kuwepo nchini humo.

"Tunawaomba wateja wetu ambayo akaunti zao hazifanyi kazi wazifungue katika muda huu uliobaki wa promosheni hii ili waweze kushiriki na kushinda zawadi hizo pamoja na safari hiyo" alisema Zawadi.

Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo, Yusuph Achayo , aliwaomba wateja wa Benki ya NMB kuendelea kutumia huduma hiyo ili kujiweka katika nafasi kubwa ya kuibuka mshindi na kwenda kula bata Dubai.

Katika droo ya kwanza wateja 100 wa Benki hiyo walifanikiwa kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja huku wengine sita wakijishindia simu hizo za 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 300.

KAWAIDA:- Na Mwandishi Wetu WATEJA sita wa Benki ya NMB wamejishindia simu janja 'Samsung S9+' baada ya kuchezeshwa droo ya nane ya shindano la Benki hiyo ya kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Washindi hao wapya wanakamilisha idadi ya washindi 12 hadi sasa waliojishindia simu kama hizo katika shindano hilo. Washindi walioshinda na kujinyakulia simu hizo wametajwa kuwa ni Taha Karimjee kutoka maeneo ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, Gladys Gilbert, Salim Abdallah, Raphael Schuurmans wa Masaki jijini Dar es Salaam, Imara Noah wa Meatu na Burton Anyisile wa Kahama mkoani Shinyanga. Akizungumzia kuhusu promosheni hiyo Meneja wa Benki hiyo Tawi la Sinza Mori, Mnkande Zawadi alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi za simu hizo. Alisema katika droo ya mwisho washindi watatu watapata ofa ya kwenda kula 'Bata' Dubai huku wakiambataba na mtu mmoja wa kila mshindi ambapo jumla yao watakuwa sita na gharama zote za safari hiyo zitalipwa na benki hiyo kwa siku nne watakazo kuwepo nchini humo. "Tunawaomba wateja wetu ambayo akaunti zao hazifanyi kazi wazifungue katika muda huu uliobaki wa promosheni hii ili waweze kushiriki na kushinda zawadi hizo pamoja na safari hiyo" alisema Zawadi. Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo, Yusuph Achayo , aliwaomba wateja wa Benki ya NMB kuendelea kutumia huduma hiyo ili kujiweka katika nafasi kubwa ya kuibuka mshindi na kwenda kula bata Dubai. Katika droo ya kwanza wateja 100 wa Benki hiyo walifanikiwa kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja huku wengine sita wakijishindia simu hizo za 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 300.

No comments: