Advertisements

Friday, March 22, 2019

MAAFISA HABARI WA SERIKALI WATOA MSAADA WA WA MIL. 7.5 KUWASAIDIA WAZEE BUKUMB


Afisa Mfawidhi wa Makao ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi Bi.Leah Mwakatobe akitoa neno la shukrani kwa Uongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) baada ya kuwatembelea na kuwapa msaada wa Magodoro, Mashuka, Vyandarua, Mabeseni, Vyandarua ,Mchele na Mafuta.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Habasi akizungumzia jinsi Maafisa Mawasiliano walivyoguswa na Kuamua kuwasaidia Wazee wa kituo cha makao ya wazee na wasio jiweza kilichopo Bukumbi Wilayani Misungwi walipowatembelea leo katika eneo la Bukumbi Wilayani Misungwi

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Maafisa Habari wa Serikali wametoa msaada wenye thamani ya jumla ya shilingi 7, 507,700 katika Makao ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Bukumbi jijini Mwanza.

Misaada hiyo imetolewa jana ikiwa imejumuisha vitu mbalimbali vikiwemo vyandarua 88, magodoro 88, mashuka 176, mabeseni 88, mchele kilo 110 na mafuta ya kupikia lita 40 vilivyogharimu jumla ya shilingi 6,085,700 huku fedha taslim shilingi 1,422,000 zikichangwa papo kwa papo.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali ya Awamu ya Tano inafanya juhudi mbalimbali za kuwasaidia wazee nchini.

“Kwa kuwa serikali inaendelea kuboresha maisha ya wazee wasiojiweza walioko katika makazi yao, na kwa kuwa Maafisa Habari wa Serikali ni moja ya wanaounga mkono juhudi hizo, kwa pamoja tumeamua kuja kwa ajili ya kuwasaidia wazee hawa”, alisema Dkt. Abbas.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amesema kuwa jukumu la kulinda wazee ni la jamii nzima hivyo anawashukuru Maafisa Habari wa Serikali kwa kuamua kwenda kuwatembelea wazee hao.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza, Leah Mwakajobe amefafanua kuwa makazi hayo yana jumla ya watu 88 ambapo kati ya hao wazee ni 73 na watoto ni 15.

“Kwa kuwa serikali inawajali wazee na kuendelea kuwapa misaada mbalimbali, natoa rai kwa wananchi kuwapenda na kuwajali wazee hao kwani baadhi yao waliitumikia nchi hii kwa nguvu zao zote,”alisema Bi. Leah.

No comments: