Advertisements

Tuesday, June 18, 2019

Rais Magufuli amtengua Mwenyekiti Bodi ya REA

By Baraka Samson. Mwananchi

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amefanya mabadiliko usiku huu kwa kubadilisha uongozi wa juu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REA, Michael Nyagoga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa usiku huu, Rais Magufuli amemteua Wakili Julius Kalolo kushika nafasi hiyo kuanzia leo Jumatatu Juni 17, 2019.

No comments: