Advertisements

Tuesday, June 18, 2019

Rais Morsi azikwa Cairo


Cairo, Misri. Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohammed Morsi amezikwa mjini Cairo siku moja baada ya kufariki dunia.

Rais Morsi alifariki dunia jana Jumatatu Juni 17, 2019 baada ya kuanguka mahakamani alipokuwa akisikiliza kesi yake.

Televisheni ya Serikali ya Misri iliripoti kuwa Morsi alidondoka mahamani hapo muda mfupi baada ya kusikilizwa kwa kesi yake na kufariki dunia baada ya muda mfupi.

Mwanasheria wa kiongozi huyo, aliliambia Shirika la habari la AFP kuwa Morsi amezikwa na familia yake leo Jumanne asubuhi June 18, katika eneo la Mashariki wa mji wa Cairo.

Awali mtoto wa kiongozi huyo, Abdullah Mohamed aliliambia Shirika la habari la Reuters kwamba maafisa wa Serikali walikataa maombi ya familia ya kiongozi huyo kumzika kijijini kwao katika maziko ambayo yangehudhuriwa na wanafamilia na majirani zake.

Morsi (67) alikuwa kizuizini toka mwaka 2013 mara baada ya jeshi la nchi hiyo kupindua utawala wake.

No comments: