ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 17, 2019

Simulizi ya maisha ya watoto waliobebeshwa mzigo wa malezi

By Rehema Matowo, Mwananchi rmatowo@mwananchi.co.tzgmail.com

Saa moja asubuhi naanza safari ya kwenda kijiji cha Nkome kata ya Nkome katika halmashauri ya Geita. Takribani kilomita 60 kutoka Geita mjini, lengo ni kufika Shule ya msingi Mwaloni, shule inayodaiwa kuwa na utoro wa wanafunzi kwa asilimia 20.

Saa tatu asubuhi nafika shuleni hapo na kupokelewa na mwalimu mkuu, Juma Henry ambaye ananieleza hali halisi ya shule na sababu zinazochangia utoro.

Mwalimu Henry anasema uwepo wa Ziwa Victoria katika eneo hilo licha ya kuwa fursa ya kiuchumi, lakini limegeuka kuwa janga kwa watoto hasa wazaliwa wa kwanza ambao wanabebeshwa majukumu ya kuwalea wadogo zao baada ya wazazi kuhamia visiwani kwa ajili ya kutafuta kipato.

Kijiji hicho kinazungukwa na visiwa vya Migongo, Izumachel na Rubaragasi.

Katika Shule ya Mwaloni yenye wanafunzi zaidi ya 2,800 wanafunzi zaidi ya 40 wanaishi bila ya wazazi au walezi huku wakiwalea wadogo zao baada ya wazazi wao ama kutengana au kuhamia visiwani.

Kwa kawaida mtoto wa miaka tisa hadi 13 anatakiwa kuwa darasani akikuza ubongo wake na anahitaji kusaidiwa, kulelewa, kukuzwa na kupewa mahitaji ya msingi kutoka kwa wazazi au walezi wake.

No comments: