
Mke wa marehemu Charles Wandwi, Kittoshe (katikati) na waombolezaji wengine wakiwa msibani. Marehemu Charles ameacha mke na mtoto wa miezi minane.
NI pigo kubwa kwa tasnia ya habari, wanafamilia na Azam TV kwa kuondokewa na wafanyakazi watano waliofariki dunia jana Jumatatu, Julai 8, 2019, katika neo la Kizonzo katikati ya Igunga, Tabora na Sheuli , mkoani Singida baada ya gari lao aina ya Coaster kugongana uso kwa uso na lori wakati wakielekea kwenye uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi huko Chato.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deo Rweyunga, wakiwa katika ofisi za Azam Media kwa ajili ya kuwaaga marehemu.

Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa na wadau wa habari na michezo wameungana na wanafamilia na waombolezaji kuwaaga marehemu hao.

Global TV Online itakuwa LIVE kukuletea matukio yote yatakayojiri katika tukio hilo la kuwaaga marehemu.


Mmiliki na Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa (wa pili kulia), akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwenye shughuli ya kuwaaga wafanyakazi watano wa Azam Media.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa (kulia) akisaini kitabu cha maombolezo.

Magari ya kubebea miili ya marehemu yakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kuipeleka ofisi za Azam Media Tabata kwa ajili ya kuagwa.

Katibu mkuu wa shrikisho la soka nchini (TFF), Wilfred Kidao, akisaini kitabu cha -maombolezo GPL
No comments:
Post a Comment