ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 4, 2019

Mahaba: Punguza Moto Wali Uive

HALOOOO eeeehhh shoga wanakwambia mjini raha jipe mwenyewe, hata kama mtu mzima nunua pampas kisha jikojolee, kwani bei gani! Unajifanya kuvaa viatu virefu wakati hata ndala ya msalani huna! Shoga usiwe kama pipa lililokosa mfuniko maana kila taka itarushiwa humo! Unajifanya kulingia uzuri wakati kwa wanaume wanakukimbia kisa umbo la michelini, umbo lisilo na shepu! Heee heeeiyaaaa acha wenye uzuri wetu tulinge, wenzio tuna utamu wa kuku tunatafunwa hadi mifupa, upo nyonyo?

Leo nipo na wewe mwanamke mwenzangu ambaye hujui harufu ya chumbani ipoje, ya sebuleni hadi ya nje.. wee kutwa kunuka moshi kama mchoma mkaa! Jamani ifike mahali basi tuwe tunabadilika, kuna vitu hadi unajiuliza huyu atakuwa amejitakia mwenyewe!

Si unanijua tena mwenzako nilivyo, hakuna linalonipita bure! Umri unakwenda shoga, usipobadilika ukiwa kijana usitegemee kubadilika ukizeeka! Hivi huoni haya wenzako wakiwa na utamu wa samaki wanaliwa hadi miba wakati wewe mwenyewe unakimbiwa kama gari la taka? Ngoja niwape somo nyie msiofundwa mkafundika! Najua wengi mmepitia hii hatua na kuona ni mambo ya kizamani, mwisho wa siku mnakuja kujiaibisha, siku mbili tatu huyoo amerudi nyumbani kumbe mchawi ulikuwa wewe mwenyewe!

Shoga juzi nimemshuhudia mwanamke mwenzangu ambaye nilisoma naye chuo kimoja, yaani kwanza nilivyomuona akataka kunipeleka hadi kwake anapoishi, looo! Nilichokutana nacho, bora niteme mate yataliwa na bata kuliko kukaa nayo yakanipalia!

Mwanzoni nilijua huenda ni pilikapilika ndiyo maana ile harufu naisikia, alipoenda kubadili nguo ndiyo kwanza nikasema kimoyomoyo bora angebaki vilevile tu! Shoga anatema; si kwapa, si shingo, si kiuno wala nguo alizokuwa amevaa!

Kama unavyonijua shosti, mimi tena, si wa kukaa nalo walaa! Nikamhoji kulikoni shoga hata kutumia pafyumu, au hata kujifukiza? Nikamuona amekuwa mpole kama kuku akitaka kutaga na kuanza kuniambia sasa! Ohh ameamua kuwa singo mama, kila mwanaume anayempata anampa mimba na kumuacha akiwa bado na mtoto mdogo!

Anasema hakuna kitu anachokichukia kama jasho lake, akitoka tu hata kama ni nje ya nyumba na kurudi, basi atanuka kama yai viza. Nikaanza kumpa somo sasa kama kweli anataka wali uive, basi sharti apunguze moto! Yaani ahakikishe kwanza anakuwa msafi wa mwili na siyo kila manukato basi ni mazuri, kwani mengine yanaongeza harufu mbaya!

Nikamwambia asiwe kama mlango wa choo unapigwa hodi kukiwa na dharura tu tena dharura yenyewe ya uharishoo! Shuuutuuuu! Mwanamke kujitambua, usiache nguo chafu ukairudia tena, hakikisha makwapa, sehemu za babaa hizo zinakuwa safi muda wote, upo nyonyo?

Kwa leo nisiwe muongeaji saana, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi. Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu.GPL

No comments: