Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo ambaye ndiye mgeni rasmi ,akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Habari Maalum kilichopo Ngaramtoni mkoani Arusha .
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani nArusha Cloud Gwandu akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika chuo cha Habari Maalum.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele pamoja na viongozi wa chuo cha uandishi wa habari na uongozi cha Habari Maalum Media.
Na Vero Ignatus,Arusha
Waandishi wa habari mkoani Arusha chini ya chama cha waandishi wa habari mkoani hapo( APC)Wamehitimu mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji na utayarishaji na video na uzalishaji yaliyoandaliwa na chuo cha Habari Maalum Media lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika kuyatimiza majukumu yao ya kila siku.
Mafunzo hayo yamehusisha utayarishaji wa miradi,upigaji picha,uaandaaji wa picha ,kuhariri na uzalishaji wa vipindi mbalimbali vya mtandaoni sambamba na kurusha vipindi mbalimbali katika mitandao ya kijamii.
Astele Reuben Ndaluka ni Kaimu mkuu wa chuo hicho amesema kuwa waandishi wanaoyo nafasi pana katika kuielimisha jamii,kuihabarisha ,sambamba na kuijkosoa pale inapostahili kufanyiwa hivyo bila kuvunja sheria na taratibu za nchi.
Ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kujitoa kwaajili nya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika nyanja tofauti ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko yaliyopo kwa sasa ya sayansi na teknolojia huku akiwaasa wahitimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kiuandishi.
Willy Chambulo ni Mwenyekiti wa TATO amewasisitiza wahitimu wa mafunzo kuwa na matumizi sahihi ya elimu waliyoipata na kuahidi kuendelea kusaidia waandishi wa habari watakao kuwa na utayari kupata mafunzo zaidi.
Aidha amewataka kuitumia vyema elimu waliyoipata sambamba na kuigeuza kuwa pesa ili ilete manufaa kwa jamii na kuepuka kuwa tegemezi
Cloud Gwandu ni mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha ,ameishukuru TATO kwa kufadhili mafunzo hayo ya kozi fupi kwa waandishi hao, na kuahidi kuwa mafunzo hayo hayataishia darasani ,bali watayaweka kwenye vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Gwandu amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu,ambapo kundi lingine la waandishi wa habari litapata mafunzo hayo baadae mwezi huu ,lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuwa na weledi katika kutaarisha kuandaa habari mbalimbali ya matukio katika jamii kwenye mitandao ya kijamii
Amesema waandishi wa habari wanayo nafasi pana ya kwa kutumia mitandao ya kijamii ,kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya utalii ,haswa kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivituo mbalimbali vilivyo nchini
No comments:
Post a Comment