Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adlof Ndunguru, na kulia ni Mchumi Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dionisia Mjema.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza kuongezeka kwa wigo na fursa za upatikaji wa huduma za fedha kwa wananchi utakao tokana na Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, katika Kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema, akitoa mada katika Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, uliofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, wakifuatilia kwa makini maagizo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu Sekta ya Fedha kuchangia katika uchumi wa nchi.
Wadau kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia majadiliano ya uboreshaji wa rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, uliofanyika Jijini Dodoma.
Wadau wa Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema. (Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)
No comments:
Post a Comment