MAWAZIRI wa Afya wa Nchi za SADAC wametembelea Bohari Kuu ya Madawa jijini Dar es Salaam ili kujionea shughjuli mbalimbali zinazotekelezwa na Bohari hiyo.
Katika ziara hiyo Waziri wa Afya, Mher. Ummy Mwalimu ndiye aliyewaongoza mawaziri hao kutembelea Bohari hiyo kubwa kabisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
“Asubuhi ya leo nimeongoza Mawaziri wa Afya wa SADC kutembelea Bohari ya Dawa ili kujionea kwa macho uwezo wa MSD ktk kununua, kutunza na kusambaza dawa kwa ajili ya nchi za SADC.” Ameandika Waziri Ummy Mwalimu katika ukurasa wake wa Facebook leo hii Novemba 8, 2019.
Waziri Ummy amesema….mwaka 2018, Mawaziri wa Afya wa SADC katika kikao chetu mjini Windhoek Namibia kwa kauli moja tulipitisha MSD kununua na kusambaza Dawa kwa ajili ya nchi za SADC. Utaratibu huu utawezesha dawa kupatikana kwa bei nafuu
Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu wa pili kulia akiwa na Mawaziri wa nchi za SADC 2019 wanaoshughulikia masuala ya Afya wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bw.Laurent Bwanakunu (kulia) alipokuwa akitoa maelekezo kwa wageni hao walipotembelea Bohari ya Dawa leo kujionea hali halisi ya dawa nchini Tanzania
No comments:
Post a Comment