Advertisements

Friday, November 29, 2019

Sumaye Apigwa Chini Chadema

ALIYEKUWA mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya ‘hapana’.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Alhamisi, Novemba 28, 2019, mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1995 hadi 2005 amepigiwa kura 28 za ndiyo na 48 za hapana na kura moja imeharibika.

Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Patrick Ole Sosopi, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Sumaye amesema lililofanyika ni demokrasia japo hana uhakika kama kutoa adhabu kwa mtu aliyekuwa anatumia haki yake kufanya demokrasia ni sahihi.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe na wanachama waliokuwepo walilipuka kwa shangwe huku wakiimba nyimbo mbalimbali za chama.

Sumaye huenda akakacha kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwani ametoa kauli akisema licha ya kuchukua fomu ya kugombea lakini hajaijaza, hivyo anafikiria ama aijaze au aichane. Amesema alichukua fomu ili kuonesha kuna demokrasia ndani ya chama hicho, na si kweli kuwa nafasi ya Mwenyekiti haiguswi GPL

No comments: