Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia akihutubia adhira iliyojitokeza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mbegu za korosho jimbo la Mongu, Zambia tarehe 16 Novemba, 2019
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi shehena ya mbegu za korosho kwa Serikali ya Jamhuri ya Zambia katika hafla iliyofanyika mjini Mongu nchini humo.
Korosho hizo zimekabidhiwa kufuatia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe.
Edgar Lungu kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pamoja cha
Huduma Mpakani (OSBP) Tunduma tarehe 5 Oktoba, 2019.Katika tukio hilo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na
kwa upande wa Zambia, Serikali aliwakilishwa na Waziri wa
Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita, Watendaji kutoka Serikalini na viongozi wa Kimila.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kapita kwa naiba yaSerikali ya Jamhuri ya Zambia ametoa shukurani za pekeewa Mhe. Rais Magufuli kwa upendo aliouoneshakwa Zambia na kwa upekee kabisa kwa wananchi wa jimboa Mongu.
Aliongezea kusema wananchi wa Mongu wanamatumaini makubwa kuwa, mbegu hizo zitawapa
chachu ya kuzalisha korosho kwa wingi na kunufaika kiuchumi kama ambavyo imekuwa kwa wananchi waTanzania
Waziri wa Jimbo la Mongu, Zambia Mhe. Richard Kapita akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na Mhe. Mukela Manyindo Waziri Mkuu wa Jimbo la Mongu (katika ngazi ya kimila) wakikata utepe kuashiria mapokezi ya mbegu za korosho katika hafla iliyofanyika Mongu, Zambia
Picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi mbegu za korosho
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia (kushoto) na Afisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia wakifuatilia tukio lililokuwa likiendelea wakati wa hafla ya kukabidhi mbegu za korosho
Shemu ya wananchi wa Mongu, Zambia waliojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho
No comments:
Post a Comment