ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 20, 2019

WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA SADC KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA KAZI NA AJIRA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wataalamu waliohudhuria mkutano wa SADC wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane akieleza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe akizungumza wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (kushoto) kwenye meza kuu akisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane (hayupo pichani). Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe, Mwakilishi wa Vyama vya Kibiashara vya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Michael Akuupa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) waliohudhuria mkutano wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

No comments: