Advertisements

Friday, December 6, 2019

KATIBU MKUU MWALUKO ATETA NAMKUU WA MKOA MWANZA MAANDALIZI SHEREHE ZA UHURU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimueleza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, juu ya umuhimu wa kukamilisha kwa wakati shughuli zitakazo fanyika siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe hizo leo, tarehe 5 Desemba, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Mkuu mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher Kadio, leo, tarehe 5 Desemba, 2019, wakiwa katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo 
Kikundi cha Kwaya cha MVC kikifanya mazoezi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, leo, tarehe 5 Desemba, baada ya kukagua shughuli za maandalizi za Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019, katika viwanja vya CCM Kirumba. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, leo, tarehe 5 Desemba, 2019 akishuka katika jukwaa la Uwanja wa CCM Kirumba, mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi za Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.

No comments: