Mchezaji wa Kikapu Kobe Bryant akiwa na mwanane Gianna Bryant wote wawili walipoteza maisha kwa ajli ya helkopa siku ya Jumampili asubuhi Jan 26, 2020.
Jan 26, 2020 ilikua ni Jumampili iliyoanza kama jumapili zingine kwa familia ya Bryant. Kobe na mwanae Gianna ni dhahiri waliamka wakiwaza mpira wa kikakpu katika vichwa vyao.
Kobe amezoea kutumia usafiri wa helkopa mara kwa mara ndio usafiri wake mkuu anapokua Califonia anaoutumia, mbali ya yeye na mwanae kulikuwepo na rubani na watu wengine 6 waliokuwemo ndani ya helkopta hiyo iliyofanya jumla ya watu 9 ambao wengine majina bado hayajatajwa bado. Ilikua ni Jumapili iliyoghubikwa na majonzi ya kumpoteza baba na mwanae, Kobe akipoteza maisha akiwa na umri wa miaka 41 na mwanae akiwa na umri wa miaka 13.
Saa 10:30 jioni Utabili wa hali ya hewa (L.A.weather) walitangaza kuwepo kwa ukungu mwingi uliosababisha hata helkopa za polisi kuzuiwa kuruka kutokana na hali hiyo ya hewa kuwa na ukungu mwingi, Mnara wa kuongezea ndege ulisema rubani wa helkopa ya Kobe iliripoti kukumbana na hali ya hewa mbaya. Kwa mujibu wa taarifa hiyo rubani wa helkopa alishindwa kuendelea na safari alipofika eneo la kuhifadhia wanyama la L.A. zoo na alishusha helkopta chini kwenye atitudi ya futi 875 huku akizunguka eneo hilo takribani mara 6 kusubili ukungu kupungua.
Wanachojua rubani wa helkopa aliwasiliana na mnara wa kuongozea ndege wa uwanja wa ndege wa Burbank mida ya saa 3:30 asubuhi, mnara wa waongozaji ndege ulikua na taarfika ya rubani wa helkopa ya Kobe alikua akizunguka eneo hilo takribani dakika 15. Baadae ruban aliekea kufuata barabara ya mwendo kasi ( highway namba 118) kaskazini na kubadilisha uelekeo na kuelekeza helkopta kufuata barabara ya mwendo kasi (highway namba 101) kuelekea magharibi ya barabara hiyo.
Takribani saa 3:40 asubuhi. ukungu ulizidi kuongezeka na kumfanya rubani kuelekeza helkopa kuelekea kusini na ndipo alipojikuta akielekea kwenye milima na rubani kupaa juu kutoka futi 1200 mpaka 2000.
Baadae takribani saa 3:45 asubuhi rubani akiruka juu ya mlima akiwa futi 1700 na mnara wa kuongozea ndege ulinasa wakienda kwa mwendo wa 161 knots. na hapo ndipo ilipokua mwisho wa maisha ya Kobe na mwanae na watu wengine 7 akiwemo rubani wa helkopta. Mungu alilaze roho za marehemu pema peponi, Amina
No comments:
Post a Comment