Kosa hilo la kubaka alilifanya katika eneo la Kasoko Ujiji mnamo Aprili 23, 2019, wakati mtoto huyo akipatiwa matibabu nyumbani kwake kinyume na kifungu cha 130 na kifungu kidogo cha 1 (E).
Awali, mashahidi wanne akiwemo mtoto, mama, daktari na mpelelezi wa Polisi uliwasilishwa mahakamani hapo kuhusiana na tukio hilo, ambapo ushahidi wa daktari ulibainisha mtoto huyo kuwa alibakwa huku mshtakiwa akijitetea kutohusika na kitendo hicho.
Wakili wa Serikali, Raymond Kimbe, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kama sheria inavyosema, ili iwe fundisho kwa watu wengine huku mshtakiwa akijitetea mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza.
Baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Kitalo Mwakitalu, kujiridhisha na ushahidi wa mlalamikaji pasina kuacha shaka alimhukumu kwenda jela maisha.
GPL
No comments:
Post a Comment