ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 26, 2020

MILIONI 117 ZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA ZAPATIKANA BAADA YA WAZIRI KIGWANGALLA KUHAMASISHA WANANCHI LONGIDO.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akivishwa Vazi la heshima la Kabila na kupewa jina la Kimasai kama ishara ya kutambua mchango wake katika shughuli za Uhifadhi na utatuzi wa kero na migogoro mbalimbali ya wananchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine wilayani Longido ambapo jumla ya shilingi milioni 117 zimepatikana.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine wilayani Longido ambapo jumla ya shilingi milioni 117 zimepatikana.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa mara baada ya kuendesha Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ketumbeine wilayani Longido ambapo jumla ya shilingi milioni 117 zimechangwa na wananchi na wadau mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea fimbo ya heshima kutoka kwa mzee wa Heshima wa kabila la Masai kwa kama ishara ya kutambua uchapakazi wake na mchango anaoutoa katika shughuli za uhifadhi hapa nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ketumbeine, wilayani Longido ambapo jumla ya shilingi milioni 117 zimepatikana na kuvuka lengo lililowekwa la kukusanya shilingi milioni 100.
Harambee hiyo imehusisha wananchi wa Kata hiyo ambao ni wafugaji wa Kabila la Masai, Mbunge wa jimbo hilo Dkt.Steven Kiruswa , viongozi wa Halmashauri ya Longido, mashirika, wadau mbalimbali wa maendeleo na Taasisi za Uhifadhi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwa Kata hiyo ina maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya shughuli za uhifadhi wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa Harambee hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla ambaye alikua mgeni rasmi amewapongeza wananchi wa Kata hiyo kwa kujitolea na kuwataka waendelee kushiriki na kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo inayoanzishwa na kutekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt.John Pombe Magufuli.
Dkt. Kigwangalla amewaeleza wananchi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekua ikitekeleza na kukamilisha kwa vitendo miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, miradi ya maji, umeme na huduma za afya, elimu.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa kupatikana kwa fedha hizo kutawawezesha wananchi wa kata hiyo kukamilisha jengo la kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje, kuwezesha upatika aji wa huduma za upasuaji, huduma ya mama na mtoto hivyo kuondoa adha ya muda mrefu ya wananchi kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 90 kufuata huduma za afya.
" Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ni Serikali inayoahidi na kutekeleza, haya yote yanayofanyika ni kwa sababu Rais wetu anachapa kazi, nawaomba muendelee kumuunga mkono na kumuombea dua Rais wetu ili aendelee kutetea maslahi ya wananchi" Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Steven Kiruswa akizungumza mara baada ya kukamilika kwa harambee hiyo amemshukuru Waziri Kigwangalla kwa kuwaunga mkono wananchi wa Kata ya Ketumbeine ambao kwa asili ni Wafugaji na wahifadhi wa wanyamapori kwa kuwa eneo wanaloishi lina wanyamapori wa aina mbalimbali.
Amesema kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha kazi ya ujenzi ikamilike na kuwawezesha wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu hasa Mama wajawazito na watoto kuanza kupata huduma za afya karibu.
Kwa upande wao wanannchi wa Kata hiyo wakizungumza kwa nyakati wameeleza kuwa kukamilika kwa kituo hicho ni ukombozi kwao na kwa wananchi wa maeneo ya jirani waliokua wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Wameeleza kuwa wao kama wafugaji wanaoishi katika eneo hilo ambalo lina wanyamapori wa aina mbalimbali wataendelea kuwa mstari wa mbele kulinda na kuhifadhi rasilimali na maliasili zilizopo katika eneo lao.

No comments: