Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Mkazi wa Kijiji cha Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo, wakati alipokuwa anawasili kwa ajili ya kufanya ziara, pamoja na kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko jimboni humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia) akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabiri Shekimweri (kushoto), ardhi ya Kituo cha Polisi Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, iliyokumbwa na mafuriko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Wiyenzele, Kata ya Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo. Simbachawene alipkelewa kwa shangwe jimboni humo, wakati alipowasili baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kushoto) akimpa pole Mtoto wa Kijiji cha Wiyenzele, Kata ya Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, ambaye wazazi wake wamehathirika na mafuriko yaliyotokea Kijijini hapo hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wapili kulia) daraja la Chipogoro lililokumbwa na mafuriko jimboni humo, Wilayani Mpwapwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia) akisalimiwa kwa furaha na Wakazi wa Kijiji cha Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo, wakati alipokuwa anawasili kwa ajili ya kufanya ziara, pamoja na kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko jimboni humo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
No comments:
Post a Comment