By Imani Makongoro, MwananchiDar es Salaam.Serikali ya Tanzania imetoa siku tisa kuanzia leo Jumatano kwa wadau wa soka kutoa maoni yao juu ya idadi ya wanasoka wa kigeni kwenye klabu za Tanzania.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe hivi karubuni aliitaka Baraza la Micheza Tanzania (BMT) kuandaa mwongozo utakaotumiwa na wadau wa michezo kutoa maoni juu ya idadi ya wanasoka wa kigeni katika wanaopaswa kusajiliwa na kila timu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
BMT imeeleza kuanza kupokea maoni hayo leo na zoezi litafungwa Mei 20.
Ofisa habari wa BMT, Najaha Bakari, amesema kutokana na janga la corona, hawataweza kufanya midahalo ya wadau wa michezo, hivyo watapokea maoni hayo kupitia mitandao ya Baraza la Michezo.
"Zoezi la kupokea maoni litafungwa Mei 20, maoni yatapokelewa kupitia tovuti ya Baraza, akaunti ya facebook na instagram sanjari na kwenye barua pepe ya BMT," amesema.
Mpaka sasa klabu zinaruhusiwa kusajili wanasoka 10 wa kigeni, huku klabu za Simba, Yanga na Azam ndizo zikionekana kufikisha idadi hiyo kwenye usajili wake.
No comments:
Post a Comment